REBECCA MALOPE NDANI YA WAPO RADIO FM PAMOJA NA MCHUMBA WAKE TAYARI KWA TAMASHA LA PASAKA KESHO

Rebecca Malope ndani ya WAPO Radio Fm mchana wa leo.
Angalia picha za malkia wa muziki wa gospel barani Afrika bibie Rebecca Malope wakati wa mahojiano katika kipindi cha Gospel celebration kinachoendeshwa na Silas Mbise kila siku za jumamosi ndani ya kituo cha WAPO Radio Fm cha jijini Dar es salaam nchini Tanzania.


Rebecca yupo nchini Tanzania kwa ajili ya tamasha kubwa la pasaka lililoandaliwa na Msama promotions chini ya mwenyekiti wake bwana Alex Msama litakalofanyika hapo kesho kwenye uwanja mpya wa Taifa akishirikiana na waimbaji wengine nyota kama Ephraim Sekeleti kutoka Zambia,Solomon Mukubwa kutoka Kenya,Rose Muhando,Christina Shusho,Upendo nkone,Upendo Kilahiro,John Lisu,Kinondoni Revival kwaya na waimbaji wengineo.

Katika mahojiano hayo mchana wa leo Rebecca aliongozana na mchumba wake bwana Themba ikiwa ni kama kufungua ukurasa mpya wa maisha yake baada ya mwanamama huyo kuambiwa na madaktari kwamba ana tatizo ambalo litamfanya kutopata mtoto kwa wakati ule hata baadaye hivyo kuamua kujikita zaidi kwenye huduma.

Kutoka kushoto,Aimtonga mtangazaji wa WAPO Radio,Rebecca Malope pamoja na msimamizi wa kipindi Elie John.

Rebecca akijibu maswali kutoka kwa mtangazaji Silas Mbise ambaye haonekani pichani,kulia kwake ni Elie John msimamizi wa kipindi akifuatilia kwa kina.

wakiwa na tabasamu kubwa,Aimtonga, Alex Msama mkurugenzi wa Msama promotions pamoja na Rebecca Malope.

Rebecca akifurahia jambo ndani ya studio za WAPO Radio fm.

Rebecca akimuangalia kwa tabasamu mchumba wake bwana.Themba wakati akijibu swali kutoka kwa mtangazaji.

Hudson Kamoga ambaye ni mkalimani wa Rebecca akiwa sambamba na Ephraim Sekeleti kutoka Zambia ndani ya studio.

Silas Mbise(mwenye shati jekundu)akiwa katika pozi baada ya kuikimbia mic iliapate picha na waimbaji hao.

weee umecheki pozi langu eeh,Rebecca, Ephraim wakiwa na watangazaji wa WAPO, Silas pamoja na Ai.

Sekeleti, Rebecca pamoja na Silas Mbise.

Sekeleti,Rebecca pamoja na Elie John,kijana ambaye yuko safi kila idara iwe ya ufundi, usimamizi, utangazaji wala usiulize mwe!

Sekeleti katika pozi kubwa na Silas Mbise.

Rebecca Malope na kijana David Gille mtangazaji wa WAPO Radio Fm.
Mchumba wa Rebecca bwana Themba,Rebecca Malope pamoja na watoto wa mtangazaji wa WAPO Radio Fm, Aimtonga.

baada ya mahojiano Rebecca akisindikizwa garini na kamanda Charles Mganga tayari kuondoka.

hamna shida wacha mie niloe na mvua mpaka mtumishi aingie garini. Kamanda Chalres Mganga anasema
Rebecca Malope alipowasili hapo jana uwanja wa ndege wa JK Nyerere,akilakiwa na waimbaji wenzake kutoka kushoto Ephraim Sekeleti,Solomon Mukubwa,Laura Msama(mke wa msama),Msama mwenyewe akiwa amembeba binti yake aitwaye Rebecca pamoja na Upendo Kilahiro na bintiye aliyeshika ua.(picha hii kwa hisani ya michuzi).
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.