SOLO WA KWETU PAZURI AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE HII LEO JIJINI RWANDAMtoto wa Umulisa aitwaye Aria aliyezaliwa hii leo.
                                     

Mwimbaji nyota wa kundi la Ambassadors of Christ choir nchini Rwanda,mwanadada Umulisa Yvonne Habimana amejifungua mtoto wa kike hii leo waliyempa jina la Aria.Mwimbaji huyo ameziweka hadharani picha za binti yake mchanga kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuanza kupata pongezi mbalimbali kutoka kwa ndugu,jamaa,marafiki pamoja na mashabiki wake.

Yvonne ambaye alifunga pingu za maisha  mwezi wa nane mwaka jana na mumewe mpenzi bwana Josue' Blaise Habimana huko jijini Kigali nchini Rwanda kisha kuhamia mji mwingine, hali ambayo ilimfanya kutoimba kwaya yake ya Ambassadors huku mashabiki wake kuanza kujiuliza maswali mengi kwamba mwanadada huyo ameamia wapi kwani hata kwenye DVD za kwaya hiyo zilizofuatia hayumo lakini jibu lilipatikana kupitia waimbaji wenzake walipotembelea nchini Tanzania mwaka jana pamoja nayeye mwenyewe kutoa taarifa za mara kwa mara kupitia ukurasa wake wa facebook.

Baada ya kuishi kwa muda nje ya jiji la Kigali,waliamua na mumewe ambaye pia ni mwimbaji katika kwaya nyingine kurudi jijini Kigali huku Yvonne akiiambia GK kwamba amerejea kuimba kwenye kwaya yake ya Ambassadors of Christ lakini alikuwa mjamzito hali ambayo ilimfanya kutoshiriki ipasavyo katika kwaya yake na ndiyo sababu iliyomfanya kutoambatana na wenzake ambao kwasasa wanarejea Rwanda wakitoke nchini Kenya walikokuwa kwa ajili ya huduma.

Gospel Kitaa inampongeza Umulisa ambaye ni mdau mzuri wa blog hii sambamba na mumewe kwa zawadi nzuri kutoka kwa Mungu,GK inawatakia ulezi mwema wa binti yao huyo mchanga.
Aria akiwa amelala.
Yvonne alipokuwa mjamzito kabla hajajifungua.
     
Umulisa na mumewe Josue' Habimana.
32 minutes ago 

My gift
  
                          Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.