TUMAINI SHANGILIENI CHOIR KUZINDUA DVD MPYA JUMAPILI HII JIJINI ARUSHA.

DVD ya kwanza iliyowatambulisha vyema kwaya hiyo.


Kwaya kongwe nchini ya Tumaini Shangilieni kutoka kanisa la Kianglikana la mtakatifu James Kaloleni Arusha,inatarajia kuzindua DVD yake mpya ya nyimbo za matumaini(tenzi)jumapili hii katika ibada ikifuatiwa na tamasha kubwa la uimbaji kanisani kwao Kaloleni.

Katika uzinduzi huo kwaya hiyo itasindikizwa na kwaya ya Mamajusi kutoka kanisa Anglikana la Mtakatifu Magret Majengo mkoani Kilimanjaro,kwaya nyingine ni Upendo kutoka hapo hapo Mtakatifu James, kwaya za Tumaini A na B ambazo ni kwaya ndogo zilizoanzishwa na kwaya hiyo ili kukuza vipawa vya watoto hao ambao wanaandaliwa kurithi mikoba ya wazazi wao watakapo staafu, pamoja na kwaya nyingine alikwa.

Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye album hiyo ni pamoja na Sitafuti Mali,Natumaini,Nionapo amani,na nyimbo nyinginezo ambapo DVD hii ilirekodiwa live na kampuni ya Mtangoo Visual Lab inayomilikiwa na mmoja wa wanakwaya na kiongozi wa kwaya hiyo ambaye ndiye aliyerekodi video ya UNISHIKE ambayo ni kati ya video zilizorekodiwa kwa ubora kwa upande wa kwaya nchini.Baada ya uzinduzi jumapili hii kwaya hiyo inajiandaa kuingia jijini Dar es salaam mwishoni mwa mwezi kwa uzinduzi mwingine rasmi.
Kwaya ya Tumaini mpaka sasa ina DVD tatu ambapo itakayozinduliwa jumapili itakuwa ya nne.
Baadhi ya waimbaji wanawake wa kwaya ya Tumaini Shangilieni.


Waimbaji wa Tumaini A juniors,wakiwa kwenye recording wimbo wao ambao utapatikana kwenye video ya Tumaini kubwa ama shangilieni wenyewe.

Baadhi ya wapigaji wa Tumaini choir wakiwa mazoezini kanisani kwao,anayepapasa kinanda ni Elkana Mtangoo.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.