NAMNA YA KUKATAA KUFANYA MAPENZI (NGONO) KABLA YA WAKATI


Mpango wa Mungu ni kuona watu wanaoshiriki tendo la ndoa ni wale ambao wamehalalishwa kuwa mke na mume na kupatana kuishi pamoja mpaka kifo kitakapowatengenisha, na hapo ndipo watu hao wanapofurahia mpango timilifu wa kuwa pamoja na ndiyo kitu ambacho kinafanya kwa watu ambao hawako kwenye ndoa kusubiri ili waje kufurahia wakati wao utakapofika.

Tendo la ndoa linapofanywa nje ya mpango wa Mungu aliouweka, mara nyingi kinachotokea kwa watu ni kupata magonjwa yasiyotibika mahospitalini, au kupoteza heshima mbele za watu wanaokuzunguka, pia kupata mimba zisizotarajiwa na hatimaye kupata mtoto au watoto nje ya ndoa jambo ambalo pia linakufanya watu wakutafsiri wawezavyo wenyewe kutokana na kwamba ulichotenda kimeonekana na ushahidi upo si kama wenyewe ambao dhambi zao wanazificha machoni kwa watu lakini Mungu anazijua.

JE MAPENZI (NGONO) NI JIBU?

Baadhi ya vijana wanaamini kwamba mapenzi yanawafanya wajisikie vizuri, wamekamilika(hususani kwa vijana wa kiume), yanawafanya wajisikie wanapendwa, wamekuwa lakini tatizo linakuja baada ya tendo lenyewe kwani ile tamaa inazidi kuwaka myoyoni mwao ili watende tena na tena si kama walivyofikiria kwamba watafanya mara moja tu. Kwahiyo kufanya tendo hilo hakusaidii kuzima tamaa zilizondani yao.
Mapenzi sio jibu lakukufanya upendwe ama upende mtu na kuzima tamaa zako za mwili na mengineyo.

BADO HUJACHELEWA!

Yawezekana unawaza kwamba kwasababu umefanya tendo la ndoa kabla ya wakati basi hakuna haja ya kusubiri mpaka ndoa, pia yawezekana unaumia kwa kile ulichokifanya na hujui namna ya kuondokana na jambo hilo, bado hujachelewa unaweza kusahihisha makosa yako kwa kumruhusu Mungu akuongoze, kwa kumuomba akusamehe na kukusafisha kwa damu yake naye atafanya hivyo ukimaanisha kutoka moyoni mwako.
Mungu akikusamehe anasemehe yote na kukukubali vile ulivyo without strings attached, there's nothing that will ever change that, even kama ulifanya tendo la ndoa kabla ya wakati.

Bado Mungu anakuwazia yaliyomema katika maisha yako, Ni kweli Mungu aliweka tendo la ndoa toka alipoumba ulimwengu, lakini mpango wake ni kwamba tendo hilo litakuwa kama zawadi kwa wapendanao mke na mume, fanya uamuzi leo kumfuata Mungu na kumuomba msamaha kwa kufanya tendo hilo nje ya mpango wake kwani atakufanya mtu mpya, kiakili,nafsi pamoja na kiroho ingawa kimwili hutakuwa kama vile ulivyokuwa awali (bikra), Mungu atakufanya kwa namna ambayo hata watu wengine ambao walikudharau ama kukubeza kugundua kitu cha tofauti kutoka kwako.

Hakuna mtu ambaye anaweza kukubadilisha kama Mungu afanyavyo na kumbuka upendo wake ni wapekee hakuna awezaye kukupenda kama atupendavyo.

NI UCHAGUZI WAKO.

Yawezekana hujawahi ama hufikirii kufanya mapenzi kabla ya wakati au unamawazo yakufanya hivyo, kikubwa GK inaweza kukuambia ni kwamba wakati huu ni muhimu kwako kuwa na uamuzi kuhusiana na hili, kama mtu ambaye uko naye kwenye uhusiano anakuletea matatizo kuhusiana na uamuzi wako wa kusubiri kutenda tendo hilo kabla ya wakati wake, ni vyema ukaachana naye kwakuwa, kwa uamuzi wako utakuwa umempendeza Mungu, pili utapata heshima kwa watu wanaokuzunguka wakijua msimamo wako. Ukipenda unaweza kuwashirikisha rafiki zako juu ya uamuzi wako ili na wao wafanye uamuzi wa busara kwa masiha yao.NAMNA YA KUSEMA HAPANA KUFANYA MAPENZI KABLA YA WAKATI

1. Kuwa na ratiba thabiti mapema ya mambo yako na kuwa na uamuzi thabiti kwamba hautafanya tendo hilo kabla ya wakati, vinginevyo utajikuta kwenye mtego wa kufanya tendo hilo.

2. Zuia hali yakuwa mpweke bila kujishughulisha na jambo, ukijiona huna cha kufanya unaweza ukawa unapanga ratiba zako mambo ambayo ungependa kuyafanya baadaye ama siku inayofuata.

3. Jiepushe na makundi ya marafiki ambao mawazo yao muda wote ni kutaka kufanya tendo hilo ama mawazo na matendo yao na maneno yao unajua kabisa yatakusababisha ukaishia kupingua msimamo wako.

4.Kuwa na mapenzi ya kweli, kama mtu anakuja kwako na kukuambia kama unanipenda.... we malizia kwa kumwambia utaheshimu msimamo wangu wa kutokufanya jambo ambalo naliona ni kikwazo kwangu.

5.Pata msaada juu ya uamuzi wako unaouweka kwasababu itakupa urahisi kueleweka kwa msimamo wako, na msaada wenyewe ambao unahitaji ni Mungu, kwani atakupa nguvu, busara na hekima wakusema hapana.

6. Kumbuka kufanya maombi kila mara ili Mungu akupe nguvu yakutotumbukia kwenye mambo yatakayokufanya uingie kwenye jambo litakalokufanya ujute hao baadaye.


HAYA NI BAADHI YA MASWALI UNAWEZA KUJIULIZA BINAFSI AMA PAMOJA NA RAFIKI ZAKO

. Je unadhani vijana bado mapema sana kwao kujiingiza kwenye mapenzi?
. Unafikiri ni kwanini vijana wanataka kufanya tendo hilo mapema!
. Unadhani msukumo huo wakutaka kufanya tendo hilo wanaupata kutoka wapi!
. Unadhani kwakufanya mapenzi ndio kunaanzisha upendo au mahusiano ya kweli?
. Unadhani kuna umuhimu gani wakusubiri kufanya tendo hilo mpaka ndoa?
. Je umewahi kuona ama unajua matokeo ya kufanya tendo la ndoa kabla ya wakati?
. Ni kwajinsi gani maisha yako yatabadilika ikitokea ukapata moja ya matokeo ya kufanya tendo hilo kabla ya wakati?
. Unajilindaje na matukio ambayo yanaweza kukupelekea ukafanya tendo hilo kabla ya wakati?

BARIKIWA SANA, MSOMAJI WA GOSPEL KITAA TUNAKUTAKIA ULINZI WA MUNGU.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.