KESHA PAMOJA NA ANNASIMA NATHANIEL NDANI YA WAPO RADIO FM 98.0 NURU YA JAMII

Annasima Nathaniel akiwa katika pozi la mnuso.                     
Jiunge na mtangazaji wako mwanadada Annasima Nathaniel kwakumsikiliza ndani ya Wapo Radio Fm kila siku za jumatatu na jumatano kuanzia saa 5 usiku hadi alfajiri katika vipindi kama Tumshukuru Mungu ukisikiliza nyimbo za kuabudu, shukurani pamoja na maombi, kisha kipindi cha  Ipo njia kuanzia saa sita usiku ambapo unapata kupiga simu na kumtia moyo mtu anayepitia katika wakati mgumu kama wa kuwa mgonjwa, kufiwa, kukataliwa na jamii inayomzunguka, wasiwasi wa mambo kumtia moyo mtu huyo utahitaji utumie mstari au mistari ya Biblia ili kumtia nguvu zaidi.

Saa nane usiku Annasima anakuwa na mchungaji ambaye anatoa huduma ya neno pamoja na kufanya maombi kwa mtu yoyote yule atakayepiga simu moja kwa moja studioni kwahitaji la maombi, kumbuka hicho ni kipindi cha Njoo Tusemezane.

Pia jiunge naye Annasima kila siku za Ijumaa kuanzia saa 6 kamili mchana hadi saa 11 jioni kupitia vipindi mbalimbali kama salamu, mahojiano na waimbaji, wachungaji, wajasiriamali, kusikiliza nyimbo mbalimbali, habari bila kusahau neno la Mungu. Usisahau kujiunga naye kila siku za Ijumaa mchana hadi jioni ili upate kubarikiwa kupitia yale anayokuandalia wewe msikilizaji wake.

Sikiliza Wapo Radio Fm 98.0 Nuru ya Jamii uwapo jijini Dar es salaam mikoa ya Pwani, Morogoro na sehemu nyingine, lakini pia waweza kusikiliza kupitia ndani ya GK popote ulipo duniani.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.