KIUMBE CHA AJABU CHAVUTA MAELFU KANISANI DAR

Moja ya mtoto aliyezaliwa akiwa na maumbile ya ajabu.

Maelfu ya watu Jumapili iliyopita yamefurika katika  la Kanisa la RGC Glory to God Miracle Center lililopo Mbezi Mwisho Jijini Dar es Salaam, kushuhudia kiumbe cha ajabu chenye kichwa, jicho moja, mguu mmoja  na mkono mmoja kilichofikishwa Kanisani hapo.

Imeelezwa kuwa kiumbe hicho cha ajabu  kimetokana na  kuwepo kwa  uhusiano wa kimwili baina ya jini na mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la  Happy Wiliam, ambaye alikiri hadharani kwamba kwa muda mrefu alikuwa na mahusiano na mwanaume wa ajabu aliyekuwa akimtokea usiku katika mazingira  ya tata ya giza.
Gazeti Msemakweli lilipata fursa ya kukishuhudia kiumbe hicho kilicholetwa Kanisani  hapo na pia kufanya mahojiano na Bi. Happy,  ambapo alieleza jinsi alivyokumbwa na tatizo hilo.
Alisema akiwa Mkoani Shinyanga  alipatwa na tatizo la tumbo ndipo alipoamua kwenda hospitalini na baada ya kupimwa aliambiwa ana uvimbe tumboni, hivyo ni lazima afanyiwe matibabu ya upasuaji.
Niliamua kuja Dar es Salaam katika Hospitali ya Tumaini  ili nifanyiwe upasuaji kwa vile nina ndugu zangu wengi wa karibu”,  alisema Happy.

Alisema cha ajabu baada ya kupimwa aliambiwa kuwa kilichopo tumboni kwake sio uvimbe bali  ni kiumbe kisichoeleweka.
Nilipewa na dawa kwa nyakati tatu tofauti na kiumbe hicho cha ajabu kikatoka bila hata kusikia maumivu”, aliongeza Happy na kubainisha kwamba  aliogopa sana kukitazama kilipokuwa tayari kimetoka huku pia kikiwashangaza sana wauguzi.

Alisema wauguzi hao walimkabidhi  kiumbe hicho na kumshauri akaombewe kanisani, ambapo  dada yake aliyemtaja kwa jina la Mama Simbila alimpeleka katika Kanisa la RGC Glory to God Miracle Centre anakoabudu kama mshirika.
Alipotakiwa na Gazeti Msemakweli aeleze ukweli kuhusiana  na sababu za kuzaa kiumbe hicho zinazoeleweka vyema, alisema anachojua yeye kilichokuwa kikimsumbua ni uvimbe tumboni kama alivyoelezwa na madaktari waliompima  mkoani Shinyanga na sio mimba, lakini alishangaa sana alipopimwa  baadaye na kuelezwa kuwa kilichokuwa tumboni kwake ni kiumbe cha ajabu.

Hata hivyo alisema  amewahi kukumbwa na tatizo la kutokewa usiku na mtu aliyekuwa akipanda kitandani kwake na kulala naye.
Alisema  anakumbuka aliwahi kufuatwa na mtu huyo akimtaka awe mpenzi wake lakini akamkatalia licha ya kuwa akimpigia simu mara kwa mara,  ndipo baadaye akaanza kumtoke usiku.

Mchungaji wa Kanisa  la RGC Glory to God Miracle Center anakosali Happy kwa sasa Mtume Peter Rashid Abubakar  alisema akiwa katika ibada ya kubatiza waumini wake wapya, alipigiwa simu na washirika wake juu ya kuletwa kwa kiumbe hicho cha ajabu Kanisa hapo,  ndipo alipofunga safari kwenda kukishuhudia.

Alisema baada ya kuzungumza na Happy na dada yake, aligundua juu ya kilichomkumba  kutokana na ufunuo aliopewa na Mungu.
Nashukuru kwamba Mungu ameniita katika kazi yake kama Mtume ambaye awali kabla sijaokoka nilikuwa mchawi, hivyo najua jinsi ambavyo Shetani au majini yanavyofanya kazi”, alisema Mtume Abubakar.
Alisema kimsingi kupitia ufunuo huo alimweleza Happy kuwa kiumbe hicho ni matokeo ya  uhusiano wake na jini lililojivika sura na umbile la kibinadamu  hivyo ni lazima amshike sana Yesu  Kristo ili kuepukana  na nguvu za giza.


 “Natoa wito kwa wasichana kuwa makini sana wanapofuatwa na vijana wanaotaka kuwaoa kwani wengine wanaweza kuwa mashetani waliotoka kuzimu ili kuwaharibu. Ni lazima wafanye bidii za kufahamu historia zao na pia kuwa chini ya viongozi safi wa kiroho wa kuwashauri”, alisema Mtume Abubakar.
Nawatangazia wachawi kuwa sasa kazi yao imekwisha kwani Mungu ameniinua ili niwasambaratishe kuanzia hapa Dar es Salaaam. Kama kuna shida katika ndoa yako, mume wako humuelewi,  karibu katika  Kanisa la RGC Glory to God Miracle Center  ili tuombe pamoja na Bwana atatenda miujiza”, alisema Mtume Abubakar.

Kanisa la RGC Glory to God Miracle Center  linaloongozwa na Mtume Abubakar linatazamana na Stendi Mpya ya Mabasi Mbezi Mwisho katika barabara ya Mogorogo Jijini Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.