MUULIZE via GK: JOHN LISU AJIBU MASWALI


Hujambo msomaji wetu wa Gospel Kitaa, karibu katika kipengele chetu cha "MUULIZE via GK" ambacho kinakujia kila siku za jumamosi ndani ya GK kinachokupa fursa ya kumuuliza msanii ama mtumishi yeyote wa Mungu swali moja kwa moja kupitia ukurasa wa Gospel Kitaa, na kwa kushirikiana na Gospel Celebration, utayapata majibu yako kwenye kipindi. Leo John Lisu amejibu maswali ambayo umemuuliza kupitia ukurasa wetu wa facebook. Karibu usikilize sauti za majadiliano, na pia ujisomee mwenyewe hapo chini mazungumzo yote.

   • Magele Winner Wa ukonga dukani kwa bibi,john hii Jehova yu hai ni (epsod nini!) mana ulianza na Jehova yu hai audio ukiwa na wana wa asafu,ukaja na jehova yu hai dvd live,ukaja na jehova yu hai tour au tuwa,na sasa umeichaka chua kidogo umekuja na yu hai jehova,yaani jina la mbele umelileta nyuma na la nyuma umelipeleka mbele vice veiser vipi Mungu wako hana maono mapya na mbona waimbaji unaowalika ni wale wale toka miaka ile kama paster paol safari,the voice,nk,ina mana hakuna waimbaji wengine wa gosple wanaoweza kuimba mana gloryuse sio waimbaji wageni samahani lakini mambo ya binadamu naitaji kujua


JOHN LISU: aaaaa, Silas Mbise labda nianze kusema ya kwamba Jehova yu Hai, sio kwamba ni series au ni nini, lakini ni album ya kwanza, ilikuwa ni audio. kama nilivyorekodi audio ya kwanza mwaka 2006. ambayo inaitwa Jehova yu Hai na hyo Jehovah yu Hai ndo nilikuja 2008 nikafanya video yake kwa hiyo nisingeweza kuita tena jina lingine na wakati ni video ya hiyohiyo albamu moja, ambayo inajulikana kama Jehova yu Hai.

Naaa Tour, ya Jehovah yu Hai, ilikuwa ikiitwa tour ya Jehova yu Hai kwasababu tulikuwa tunafanya hiyo tour, na tunaimba nyimbo ambazo ziko kwenye albamu ya Jehovah yu Hai, kwahiyo ndo maana ikaitwa tour.. Jehovah yu Hai tour, sio kwa sababu eti Mungu watu kaishiwa, Mungu wetu haishiwi. Naa sasa hivi wimbo wa Yu Hai Jehovah nii, maneno tu yameendena, lakini ukisikia mahadhi yake ni tofauti, amaeno yaliyoimbwa humo ndani ni tofauti, kwahiyo si kwamba ni kitu kimoja ama Mungu anaishiwa.

Na kitu kingine pia waimbaji ambao ninawaalika, unajua kila mwimbaji ana watu ambao anawapenda, yanii anapenda kufanya nao huduma kwenye steji moja inawezekana anajisikia vizuri, kwa hiyo haijalishi ya kwamba hamna wengine, lakini nimejisikia kuwaalika hao kama the Voice, kama kina nani, wanafanya kazi nzuri katika muziki, na mimi ninapenda kuwapa watanzania kilicho bora. kwahiyo kama Glorious wanapiga muziki vizuri, Chidumule mzee wetu anapiga muziki vizuri, naa wanaweza wakapiga live, kwa hiyo sio kwamba ni upendeleo ama hamna watu wengine, ni kwasababu ya hivyo, concert yangu ni ya live, concert yangu sio ya CD. Kwa hiyo wanaokuja wataimba live, na waimbaji wengi Tanzania hawaimbi live, wanaimba na CD kwa hiyo inaniwia ngumu hata kama nikimuita nani, anakuja anashindwa kuimba live, amezoea CD, kwa hiyo that's why ninawaita hao ambao najua watanfaya kitu cha live kama mimi Mungu alivyoniita na wito wangu ulipo.

Nina wanamuziki ambao tayari ni wanamuziki wakubwa ambao tunafanya nao kazi. Sina bendi ya kusema hii ni bendi yangu naimiliki, lakini nina watu ambao tayari tumeshakubalinana tunafanya nao kazi, huduma ya Mungu, hao wapo ambao ndo maana unaniona napiga muziki wa live kwa sababu kuna watu kama hao. Nina watu kama kina Sam Yona, wakina Amani Kapama, wote hao wanafanya hiyo kazi ya Mungu, kwhiyo kitu kingine


  • Dotto RK Wa kigamboni DSM namuuliza John Lisu kwanini nyimbo zake zimekua ktk series inayo fanana,pili anayo bendi au kikundi,tatu jee kwanini amewekeza kufanya live na sio kwamshindo nyuma.

JOHN LISU: kuchagua muziki wa live kwasababu sitaki kumpa Yesu Makombo, eeh nataka kumpa Yesu kilicho bora, na kwa wakati huo. Sitaki kumuweka Yesu kwenye CD., naa kama naimbia CD maana ake namlimit Roho Mtakatifu kufanya kitu chochote kwa wakati wowote, kwa hiyo mimi nimeshagundua hiyo siri, na nimeamua muziki wangu uwe live, ili Roho Mtakatifu akitaka kufanaya chochote kuingilia chochote anaruhusiwa kufanya chochote kwa wakati wowote, lakini kama naimbia CD manaake ntashindwa kumruhusu Roho Mtakatifu, CD ikiisha ntamwambia Roho Mtakatifu eeh, CD imeisha kwa hiyo tulia tu tuishie hapo, lakini kama nikifanya live, maana yake namruhusu Roho Mtakatifu kufanya chochote na kunitumia jinsi apendavyo.JOHN LISU: Aah DVD zangu zinapatikana, naa nasambaza mwenyewe kwa sababu nilikuja kugundua usambaji nauweza, kama ni muda mrefu sasa hivi nimekuwa nikisambza mwenyewe, na zinaenda nimeshauza kopi maelfu na maelfu, nikajua nina uwezo kusambaza mwenyewe, kama watu wanahitaji DVD zangu basi wanitafute mimi mwenywe ndo msambazaji, watapata DVD.


  • Eliufoo Simon wa Tanga mjini, nauliza wazo la album hii lilikujaje? Nafahamu ya kwanza ilikuwa ni "pure download from heaven" na ulisema hadi bendi ilishuka kuimba Jehova yu hai..La pili, una undugu na Tundu Lisu? Ubarikiwe mtumishi...JOHN LISU: (kicheko) aaah unajua usimlazimishe Mungu kutaka kila kitu kifanane, kama alisema hivi mwanzoni, unataka arudie vilevile, Mungu ana njia nyingi za kuongea, kwa hiyo hii album imekuja ni ya Mungu, Bwana amenipa nyimbo, lakini zimekuja kwa aina nyingine. Naa pia Tundu Lissu ndugu yangu no, ni jina limeendana.JOHN LISU: (Kicheko), aaah ahsante sana Evelyn, kwa kubarikiwa na uimbaji, naaaaaaa.. sikatai ya kwamba mtu anakatazwa kuja kujiunga, lakini kuna taratibu ambazo lazima tuzichukue, kwahiyo hilo jambo limekaa kibinafsi zaidi, anaweza akaja tukaongea, tukazungumza tukaelewana.

  • Elina Gideoni Wa Tegeta basihaya, ki ukweli nabarikiwa na uimbaji wako sana John Lisu, ila napenda kukuuliza una malengo gani na bendi yako, alfu nyimbo zako nyingi ni kama za kusifu ambazo zinajulikana ila we unazifanyia modifction kwa nini?JOHN LISU: Aaa nyimbo ambazo nimezifanyia modification ni zipi inawezekana ni nyimbo amabzo nimeandika zinaimbwa makanisa mengi kwasababu nimekuwa nikiandika nyimbo zinaimbwa kwenye praise and worship makanisani kwahiyo mtu anaweza akajua kwamba John Lisu amefanya modification kumbe imetokea ya kwamba hizo nyimbo nilizoandika zinaimbwa makanisani ka! kwa mfano wimbo wa ''Uko Hapa'' ambao umebeba album umeimbwa na makanisa mengi sana kiasi kwamba walikuwa hawajui hata aliandika huo wimbo ninani, kwahiyo ime imetokea huyo dada labda amejua ya kwamba hizi nyimbo zinaimbwa makanisani kwahiyo John Lisu amefanya modification sijafanya modification ni nyimbo ambazo Mungu amenipa na hizo nimezikuta zinaimbwa makanisani kwahiyo na ni maombi yangu kwamba nyimbo ninazoandika au Mungu anazonipa ziimbwe makanisani  kwasababu mimi nafanya muziki wa kusifu na kuabudu kwahiyo na watu wakiimba makanisani mimi mwenyewe najisikia vizuri kwasababu naona ile kitu ambacho Mungu amenipa kinawafikia watu kwahiyo sio kwamba kuna nyimbo amabzo nazifanyia modification zilizoimbwa na watu hapana ni nyimbo nilizoandika Roho Mtakatifu alizonipa kwahiyo hizo zinaimbwa makanisani hata kabla mimi sijaanza kuzirekodi.JOHN LISU: E yaah Asante sana.


JOHN LISU:  Aaa men.


JOHN LISU:  Amen.


JOHN LISU:  ha ha ha(kicheko) Amen Lutu Mungu akubariki sana ukiwa huko Mwanza.


JOHN LISU: Amen

  • Danny Big-rube Silandah John Lisu your worshiper! mimi sina swali kwako sababu nayajua maono yako ktk huduma, ninachosisitiza ni wewe kukaza buti ili Africa nzima na ulimwengu wote tuwe ma-worshiper wa Mungu aliye hai! Tukopamoja rafiki yangu!


JOHN LISU: Ameen huyo Dani bwana Silas Mbise (anaita jina la mtangazaji Silas Mbise) ndio mpiga  bass(gitaa) mwenyewe ambaye anapiga bass kwenye kundi la John Lisu (kundi lake) ndio tumekuwa tukifanya naye huduma.

SILAS MBISE: Kwahiyo kesho tunampata live pia

JOHN LISU: Eee unampata live kabisa huyo.

JOHN LISU:  Aaa unajua watu wanachanganya kati ya DVD ya Sifa Zivume ya Rivers of life ya kanisa wa watu wengi wamekuwa wakijua kwamba ni ya John Lisu  lakini mimi dvd yangu mpya bado ila iko njiani baada ya kufanya launching ya hii audio tarehe 3(kesho) nitaanza kujipanga kwaajili ya kufanya live concert ambayo itakuwa ya recording ya dvd mpya yaa yake John Lisu.

SILAS MBISE:  Ok John Lisu kwa upande wa maswali ambayo wasikilizaji wameuliza na wapenzi wa Gospel Kitaa nimeishia hapo, nirudi kwa upande wangu mimi, kesho ndio siku ambayo tulikuwa tukiisubiri kwa hamu ambayo utakuwa ukiweka wakfu album yako ya ''Uko Hapa'' hebu tueleze kwa upande wa maandalizi mpaka wakati huu yamefikia wapi John Lisu

JOHN LISU: Silas Mbise maandalizi ni mazuri sana yaa yanaendelea vizuri kwahiyo toka jana sisi tulikuwa ukumbini tukifunga vyombo naa tukiweka lights na kila kitu kikae vizuri kwahiyo mambo yako vizuri kabisa maandalizi yako vizuri kabisa, wanamuziki wako vizuri, waimbaji wako vizuri naa tunatamani kukutana na Mungu kwakweli siku hii ya kesho.

SILAS MBISE: John Lisu tumezoea watu wengi wanaambiwa kwamba inaanza saa saba au inaanza saa nane lakini mtu anafika anakuta kitu kinaanza labda saa tisa saa kumi huko vipi kwa upande wa kesho unawaambia wasikilizaji tunaanza saa ngapi!

JOHN LISU: Yaani kwakweli milango itafunguliwa kuanzia saa saba ili watu waingie lakini kwakweli Silas sisi tunatazamia kuanza saa tisa kamili juu ya alama vyombo tayari jana tumeseti kila kitu mic zimesetiwa tuko vizuri, tuko vizuri watu waje tuu kwakusudi moja  la kumwabudu Mungu na kumsifu Mungu maana yeye anastahili sifa na heshima.

SILAS MBISE: Sasa hivi bado ni mapema leo ni jumamosi tumesikia tiketi zinapatikana katika vituo mbalimbali jee zimeishaa na hiyo pia kesho zitapatikanaa hebu mkumbushe msikilizaji ni wapi tiketi zinapatikana kwasasa kama anaweza kwenda kuzichukua na hiyo kesho zitapatikana hapo kanisani au vipi!

JOHN LISU: Aaa tiketi zinapatiakana Mlimani City, Silver spoon, zinapatikana Mwenge Tarakea pale kuna duka la cd's chini, tiketi zinapatikana Mbogo shop Kariakoo mtaa wa Uhuru karibu na shule ya Benjamin Mkapa, na piaa tiketi zinapatikana Kinondoni Dar es salaam Pentecostal Church yaani DPC, TX market kwahiyo pia tiketi kesho zitapatikana pia mlangoni kwa wale ambao watashindwa kabisa kununua tiketi zao leo hii kesho tiketi zitapatikana pia mlangoni lakini najua kutakuwa na msongamano sana ni heri mtu ununue tiketi yako mapema.

SILAS MBISE: John Lisu ninakuwa sina maswali mengi sana kwako unakitu gani cha kumweleza msikilizaji ambaye yupo mwingine anahamu sana na siku hiyo ya kesho.

JOHN LISU: Aaah mimi namweleza aje kwasababu aasikose yeyote anayenisikia siku hii ya leo ya jumamosi asikose siku ya kesho tena amwalike na jirani yake tena nimekuwa nikiandika kwenye page yangu ya  ya John Lisu (Facebook )ya kwamba usi usi usije mwenyewe kama wewe umesikia hizi habari hembu mwalike na rafiki yako njoo na rafiki yako naamini hataboreka atabarikiwa kwasababu lengo hasa ni nikukutana na Mungu naa tumejiandaa kukutana na Mungu hata mimi mwenyewe niko so excited kwasababu ninajiandaa kukutana na Mungu mimi kibinafsi Mungu kuyahudumia maisha yangu kwasababu nimeshazoea kwamba nikiwa madhabahuni namwambiaga Mungu anza na mimi kwanza kabla hata hujawatembelea wengine gusa kwanza maisha yangu kama nyimbo zitawagusa watu wengine hebu zianze kwanza kugusa maisha yangu. Kwahiyo watu waje wakitarajia kutoka kwa BWANA sio kwa John Lisu waje wakitarajia kutoka kwa BWANA.

SILAS MBISE: John Lisu najua kuna wasikilizaji ambao wana hamu kweli hata kuuliza tena maswali mengine ambayo mimi sijauliza kuna mawasiliano yoyote ambayo wanaweza kuyapata wakawasiliana na wewe!!

JOHN LISU: Eeee bwana wanaweza kunipigia katika namba hii 0713 240 397 hiyo namba wanaweza kunipigia kama wana maswali wakaniuliza wakanijulisha nini kinaendelea.

SILAS MBISE: John Lisu nikushukuru sana nikutakie maandalizi mema kwa ajili ya siku ya kesho natumaini kesho tutakutana pamoja katika kumtukuza Mungu wetu.

JOHN LISU: Amen Silas Mbise asante sana Mungu akubariki sana bwana ninashukuru sana na niwashukuru sana wasikilizaji waa WAPO Radio Mungu awabariki sana.

Haya hivi ndivyo tulivyomalizana na The Great John Lisu, tukutane wiki ijayo ambapo tutakuwa na kundi l a waimbaji, hawa si wengine, bali ni Glorious Celebration. Wanfahamika vema kwa nyimbo zao zinazogusa huku wakipiga nyimbo zao live. Unaweza kuwauliza swali lako hapa chini kwa kukomenti, kwa barua pepe yetu gospelkitaa@post.com au kwenye ukurasa wetu wa Facebook.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.