SPIRIT OF PRAISE YAKONGA, YASUBIRIWA JOYOUS MWEZI UJAO

                           

Wakati kundi la Spirit of Praise la nchini Afrika ya kusini likiwa limeachia dvd yake ya nne mapema mwezi huu na kuanza kufanya vizuri sokoni, wapenzi wa gospel nchini humo wanasubiria kwa hamu pia dvd ya 17 ya kundi la Joyous Celebration ambayo pia itaanza kupatikana madukani mwishoni mwa mwezi ujao hasa kutokana na waimbaji walioshirikishwa katika dvd hiyo.

Makundi hayo mawili yameonekana kuwa na upinzani wa jadi miongoni mwa mashabiki wao ambao kila mmoja kwa wakati wake husifia kundi lake kwamba ndio linalofanya vizuri kuliko jingine.

Kati ya nyimbo zinazofanya vizuri katika dvd hiyo ya Spirit of praise ni pamoja na Calvary ulioimbwa na mwanamama Zanele Fanele a.k.a Zaza ambaye alikuwa ni mwimbaji wa kundi la Joyous awali akionekana vyema kwenye dvd ya 12 na wimbo Namhla Nkosi huku album yake ya mwisho na kundi hilo ilikuwa ya 13 ambayo hakuanzisha wimbo zaidi ya kuitikia. Wimbo mwingine ni Modimo Urifile au unaweza kuuita Sebakanyana ukiwa pia umeanzishwa na kijana Kgotso Makgalema ambaye pia alipitia Joyous Celebration akirekodi wimbo Semphete na mwanadada Duduzile ambaye bado yupo na Joyous.

Kundi la Spirit of Praise hufanya usaili wa waimbaji wapya (waitikiaji) kila mwaka huku pia safu ya waimbishaji ikileta mgeni mmoja au wawili chini ya mkongwe pastor Benjamin Dube na mwanamama Zaza huku waimbaji ambao wameshashirikishwa katika matoleo mengine ni pamoja pastor Keke Phoofolo, Solly Mahlangu na wengineo.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.