MUULIZE via GK : AMBWENE MWASONGWE AJIBU MASWALI

Hujambo msomaji wetu wa Gospel Kitaa, karibu katika kipengele chetu cha "MUULIZE via GK" ambacho kinakujia kila siku za jumamosi ndani ya GK kinachokupa fursa ya kumuuliza msanii ama mtumishi yeyote wa Mungu swali moja kwa moja kupitia ukurasa wa Gospel Kitaa, na kwa kushirikiana na Gospel Celebration, utayapata majibu yako kwenye kipindi. 

Leo Ambwene amejibu maswali ambayo umemuuliza kupitia ukurasa wetu wa facebook. Karibu usikilize sauti za majadiliano, na pia ujisome mwenyewe hapo chini mazungumzo yote.

                          

Sikiliza mahojiano hapa.
Ambwene : Aaaa, mbali na music kwa kipindi hiki bado nasoma. Kwa hiyo naweza nikamjibu kwamba kwa kipindi hiki bado nasoma mbali na music.


 • Anthonia Izengo Shkamoo! kwanza hongera kwa huduma yako bro je:
  1. Kwanini unapenda nyimbo za taratibu?
  2. Nyimbo zako ni kama story je huwa zinatokea kwako au kwa wengine unaamua kuzifanyia wimbo?
  3. Unasali kanisa gani?
  Barikiwa sana kaka Ambwene na kaka Silas kip it up dearz!


Ambwene : Amina, mimiii, napenda nyimbo za taratibu namfikiri, pia ni nature ya mtu kwasababu nachoamini mtu anafanya kile ambacho kiko moyoni mwake kwa hiyo anaweza akaelewa nini nachomaanisha nikisema ni nature ya mtu pia.

Ya kuhusu stori,  japokuwa napenda kuita shuhuda. Hizi nyimboo, kwa mfano  ni nyimbo za shuhuda, za watu mbalimbali na nyingine kama zinazvyoeleza nyimbo zenyewe ni ushuhuda wangu mwenyewe, lakini sehemu kubwa ya hizo nyimbo ni matukio ambayo yametokea, na nilipenda kushirikisha watu wengine kuweza kuona kwamba kuna matukio yanayotokea si kwao peke yao, ni watu wengi yanayowakuta na hawa watu ambao nimewaimba, walifanya kitu cha ziada kwa Mungu na ikawa ni ushuhuda mzuri ambao niliona nishare na watu wengine.

Swali la tatu, kiukweli naamini katika Yesu Kristo naamini katika wokovu lakini dhehebu langu sitamwambia.


 • Rehema S. Leonard Hongera kaka kwa kazi ya Mungu unayoifanya. swali langu ni Umeanza kuimba nyimbo za injili ukiwa na umri gani? God bless You much.


Ambwene : Amina, aaa nimeanza kuimba nyimbo za injili nikiwa na umri wa miaka 16 na albamu yangu ya kwanza ya majaribu ni mtaji nimetoa nikiwa na umri wa miaka 19.


 • Magele Winner Ambwene mwasongwe leo ukipata nafasi ya kukutana na mueshimiwa Raisi ya jamuhuri ya muungano wa tanzania docta Jakaya mrisho kikwete una lipi la kumwambia kuhusiana na mustakabali mzima wa siasa za nchi yetu,uchumi,dini na sanaa ya tanzania na pia kwa niaba ya waimbaji wenzako wa injili,ungependa awafanyie nini kabla hajamaliza muda wake wa kukaa madarakani kama Raisi wa tanzania? samahani lakini mimi sio mwanasiasa


Ambwene :(kicheko) na kwasababu wewe sio mwanasiasa ngoja nianze na hili la mwisho ambalo amezungumza kuhusu maslahi ya muziki wa injili. Aah, kikubwa ambacho ningependa ningeshauri kama ningepata nafasi ya kuonana na Rais leo, ni kujaribu kuangalia ni namna gani anaweza akasaidia muziki kukua, yaani nikiongea kukua namaanisha kuhusu maslahi, wasanii wanafaidika nini na kazi zao, lakini pia nigeweza kumshauri kuona kwamba muziki wa injli peke yake una pato zuri sana kama utasimamiwa vizuri, tunaweza tukawa na nafasi nzuri ya kulipa kodi, ambayo itasaidia serikali na itasaidia jamii yetu. Kama serikali itaweka misingi mizuri ya kufuatilia ni namna gani wasanii wanafaidika na kazi zetu zinasimamiwaje ili watu wasiibe na kile kipato halisi kipatikane.


Lakini kuhusu dini, kila mmoja anafahamu kwamba nchi yetu haiamini katika dini yoyote japokuwa inaamini kuwa watu wake wana dini, ningeweza kumshauri kama ningepata nafasi ya kukutana na Rais kwamba ilie misingi ambayo imewekwa tangu awali, ya nchi yetu kutokuwa na dini iendelee kuheshimiwa na watu wote, na kama kuna haja ya kuendelea kutolewa elimu basi iendelee kutolewa kwa wanadini kutokufika mahali kwa kuamini kwamba dini moja au watu Fulani ndo wana haki zaidi kuliko watu wengine katika nchi yetu, ili amani izidi kudumu katika nchi yetu. • Davis Theobard Katonda From MADALE KWA KAWAWA. Nabarikiwa sana na uimbaji wako kaka, {i] una albam ngapi mpaka sasa? {ii] nini malengo yako katika huduma yako ya uimbaji? {iii} swali la uzushi, je kuna chombo chochote cha mziki unachoweza kuki-operate {kipi/Vipi}? Songa mbele


Ambwene : (kicheko) okeey, naomba nianze na la mwisho tena, aah nina idea kidogo ya kupiga baadhi ya vyombo, kwa mfano gitaa, aah kinanda kidogo, japokuwa gitaa hata kwenye utunzi wangu ndo mara nyingi nimekuwa nikilitumia zaidi.


Kwa sasa nina albamu tatu ya kwanza Majaribu ni Mtaji, albamu ya pili heshima ya mrefu ni mfupi na hii albamu ya tatu ambayo iko sasa sokoni,  ni misuli ya imani.


Lengo langu kwa kweli natamani kuufikia ulimwengu, sio Tanzania peke, yake kwa hiyoo, ningependa kumuomba Mungu anisaidie kuweza kuvuka mipaka hasa ya nchi yetu na kufika dunia nzima, ili kuwatia moyo watu ambao wanapitia kwenye mazingira tofauti tofauti na magumu, wazidi kusimama na kusonga mbele. • Joyce Doughty honera kaka,swali langu ni,unaimba tu Tanzania ama pia inchi zingine za east africa maana mi natika kenya,


Ambwene :Aaah, kama unavyofahamu soko letu saivi kwa East Africa, limekuwepo, mara nyingi ukikuta msanii amehit Tanzania , basi utakuta Kenya, utakuta Yganda Rwanda Burundi, anafika na Congo. Kwa hiyo kwa kujibu hivyo ni kwamba nchi zote za East Africa ninakuwa nikihudumu pia, kwa kufika na kutokufika kwa maana kawmba hata nisipofika, kazi zangu zinafika humo


 • Meckison Tenga MECKY WA G-MBOTO.mimi sina mengi ila ninampongeza kwa uimbaji wake na staili yake aliyotoka nayo nyimbo zako nazipenda sana.kaka unaweza 2nakuombea.


Ambwene : Amina, Amina.

 • Benson Mbwilo swali je?ni lini utatoa video ya albam ya pili na hii ya sasa,pia albam ya misuli ya imani kwa nini unasambaza mwenyewe na unanufaika vipi ukisambaza mwenyewe tofauti na kwa wasambazaji.mwisho umeoa maana mimi kama muuzaji wa cd napata maswali mengi kama hayo


Ambwene : ya ya ya ha ha (kicheko) okay labda ningependa kujibu lile la video na mengine nitaunganisha, videoo nitatoa na mpaka sasa hivi ninamshukuru Mungu album ya pili nimeshaanza kushoot video yake, na hii ya tatu Misuli ya Imani yenyewe ilishakamilika inafanyiwa editing ambapo ninategemea itatoka kwenye mwezi wa tano, nafikiri pia hii album ya pili  itatoka kwa kuongozana na hii album ya tatu, lakini nimekuwa nikichelewesha kutoa kwalengo moja zuri tuu  ambalo naomba watu waelewe, ujumbe wa nyimbo zangu umebase zaidi kwa mtu kusikiliza naa ndicho kitu ninachotamani moyoni  watu waweze kusikiliza na kuelewa nini ambacho kipo ndani ya hizi nyimbo ndipo baadae waje waone,

Kwahiyo hiyo ilikuwa sababu mojawapo inayofanya kuchelewa kidogo kutoa video lakini malengo na target nzuri ili watu ziwafikie zaidi waweze kusikia kwanza vizuri na waelewe halafu baadae waje waone . 

Aaah kuhusu kuoaa bado sijaoa kama nilivyosema niko shule lakini naamini ipo siku nitaoa naa namuomba huyo ndugu pia aniombee lakini yawezekana pia kwasababu anaulizwa mengi ninaweza kusema nina mtu tayari moyoni mwangu , kwahiyoo nafasi iko kama hivi imejaa ha ha ha (kicheko kutoka kwa Ambwene na Silas), 

kuhusu kusambaza mwenyewe aaah nilipenda kusambaza mwenyewe kwasababu pia unapokuwa unafanya kitu kuna hatua tunatoka kwenye udogo, utoto baadae tunakua, kwahiyo sitegemei saana  mda wote tuwe watu wakusambaziwa tuu naa nimeona nichukue hatua ya kuanza kusambaza mwenyewe naa nafikiri naona faida ya kusambaza mwenyewe si tu yakifedha lakini pia napata experience namna gani nzuri ambayo nitafanya na kusaidia watu wengine, naamini kwamba tunaweza tukasambaza wenyewe bila wasambazaji naa tukafika mahali pazuri tu. • Ruth Lister Bwana yesu asifiwe mtu wa mungu mm nina maswali mawili 
  1.Je, nyimbo zako unatunga mwenyewe au unatungiwa?
  2.unampango wowote wa kufanya kituchochote ilikusaidia jamii inayo kuzunguka? Ndo hayo tu mungu akuzidishie zaid na zaid AMINA.


Ambwene : Aminaa hizi nyimboo naweza nikasema naa kwa maana ya .... ninatunga mwenyewe kwa msaada wa Roho Mtakatifu ananiwezesha kutunga lakini kamaa anavyofahamu hizi huduma tunapozifanya ni huduma za kijamii na mara nyingi tunapoimba muziki wa injili tunakuwa tukibase zaidi kwenye jamii, kwahiyo mpango wa kusaidia watu wengine upo naninaweza kusema kwasehemu nimekuwa nikisaidia kiasi fulani kwahiyo huo mpango upo na ninachoomba tu Mungu nizidi kwamba azidi kunikuza zaidi ili nisaidie kwakiasi kikubwa zaidi ya hiki ambacho kipo kwasasa. • Edna Kunambi Shalom,je tunaipata wapi album yako mpya? Nini changamoto unazokutana nazo kwenye uimbaji wako? Studio gani unarecodi nyimbo zako.Songa mbele na kazi ya Mungu, EDNA KUNAMBI WA MKURANGA

Ambwene :Amina aah album mpya inapatikana naa naomba nitoe ufafanuzi mara zote ninaposema nasambaza mwenyewe nimekuja kugundua kwamba watu wengi wanafikiri ninazo mimi mkononi, ninaposema ninasambaza mwenyewe sio kwamba hazipatikani dukani ni kwamba mimi nasupply madukani kwa wauzaji wadogo wadogo badala ya kuingia mkataba na kampuni ambayo ingesambaza kwa wauzaji wadogo wadogo ukienda dukani inapatikana sio kwamba ninazo mimi mkononi maana yake hata dukani sijazipeleka no. 


Lakini changamoto zipo kama hii mojawapo ninayoieleza uelewa wa watu kuhusu kile ninachokifanya wakati mwingine inakuwa shida pia kuna changamoto za hawa watu wanaofanya pirates kutukwamisha nyuma sana naa nimerekodi kwaa hii album ya tatu nimerekodi katika studio mbili tofauti nimezitoa chini ya producer anayeitwa Timothy Chegula au TC na amepiga mziki kijana mmoja anaitwa Imma na studio ya pili nimerekodi inaitwa Amber record ambayo producer wake anaitwa.....(sauti haijasikika vizuri) kwahiyo lakini album zingine mbili za nyuma nimekuwa nikifanya na producer Kameta wengi wanamfahamu nafikiri.


 • Hamida Kilongo Jaman..nabarikiwa sana na kazi yako MUNGU azidi kukuinua. 
  Swali: wimbo waKo uitwao Upendo.. je, hicho ni kisa cha kweli?.
  MUNGU AKUBARIKI SANA KAKA.


Ambwene : Aminaa kama nilivyojibu mwanzoni sio tu Upendo visa vyote vilivyomo kwenye album hii ni vyakweli naa vimetokea naweza kujibu hivyo yea ni kisa cha kweli. • Dotto RK Wa kulee kigamboni DSM maswali kwa kaka Ambwene sasa,kwanini album yake hiitwe MISULI YA IMANI,inanyimbo ngapi,amefanyia studio gani,producer jee nani,hivi yeye na Ambwene Mwamwaja ni ndugu mwisho SILAS anasema ww nimpore etikweli.PAMOJA KWAUMOJA ZAIDI.

Ambwene : Aaaaaah ha ha (kicheko) aah swala la upole linategemea na nani anayeuona huo upole naa wakati gani lakini huwa naona na nasikia watu wakisema mimi ni mpole mimi sio mpole ila naomba Mungu anipe upole ambao watu wanasema ninao.

Aah album nimeamua kuiita "Misuli ya Imani" ambacho inatokana na kisa cha huyo mama aliyekuwa na watoto saba wakafa wote siku moja nikaja kugundua kwamba kuna watu ambao Mungu mara nyingi anawaamini kutokana na maneno ambayo huyu mama aliongea kwamba aliamini kwamba Mungu amemwamini ndio maana lile jambo kubwa kama hili limtokee kwahiyo kichwani mwangu roho mtakatifu akanifundisha kitu kwamba kweli kama Mungu kuna watu anawaamini kama Ayubu alivyomwamini it means wanamisuli ya kutosha ya imani, yaani ni kama kujaribu ku kuelewesha au kufafanua kuhusu imani yenye nguvu inayotenda kazi ndani ya watu katika kusimama na Mungu kwamba, inahitaji misuli ya kutosha na ndio maana nikaiita Misuli ya Imani.

(Silas (wewe na Mwamwaja mna undugu?)  aaaah nafikiri huyo kwa majina yetu ya kinyakyusa ukiona majina ya Mwa ndio yanafanana ndio kuna kuwa na undugu wowote lakini kwa kuitwa Ambwene Ambwene ni majina tu yameingiliana lakini japokuwa sisi ni ndugu wote pia kwa maana ya kuishi.
Ambwene :Hilo nimejibu • Steven Licheula KUTOKA KIBAHA TZ.AMBWENE KATIKA WAIMBAJI WLIOJISHUSHA NA KUNYENYEKEA WEWE NI NAMBA 1.JE UNYENYEKEVU HUO ULIANZA WAKATI MDOGO AU BAADA YA KUOKOKA?

Ambwene : Aaah ninamuomba Mungu anipe unyenyekevu kwasababu sina uhakika sana kama nina unyenyekevu wa kiasi ambacho alichosema kwahiyo ninamuomba hata yeye azidi kuniombea kama kuna tunda la unyenyekevu limeonekana nahitaji kuangalia katika yale yajayo mbele ili nisije nikariharibu kwahiyo ninamuomba maombi yake.
Ambwene : ha ha (kicheko) Ambwene anasoma sasa hivi katika chuo cha uhasibu kwahiyoo bado hajafika mahali anapotaka kufika ili ...... (hajasikika vizuri) • William Natai KUTOKA TEMEKE TZ, ABWENE UNATARAJIA KUPIGA NYIMBO ZA KUCHEZA LINI KWA KUWA WENGINE TUNAPENDA KUCHEZA?

Ambwene : Aaaah siwezi kusema natarajia kama Roho Mtakatifu akinipa huo ufunuo wa kuimba za kucheza nitaa nita nitafanya hivyo lakini kama Roho Mtakatifu ameniweka katika nafasi niliyopo sasa hivi nitatii na kuheshimu hiyo nafasi kama zakucheza amewapa wengine wataendelea kufanya kwa wakati wao kwahiyo hata huyo mtu akitaka kucheza naamini atabarikiwa na hao wakucheza kwahiyo ninaangalia nini Roho Mtakatifu ananipa cha kufanya. • Yeremia Enock KAK BWANA YESU NA ASIFIWE ningeomba kumuulza kak AMBWENE kam ifuatavy
  1. je anapend kuimba laiv je, kam anapend mbon jumapili iliyopit pale MITO YA BARAKA aliimba na sidii
  2.anasali wapi
  3. je, upole alionawo ulitokana na nn au ndio alivyozaliwa NA la mwisho je yeye kama yeye anampend MUIMBAJI na BENDI GANI HAP TZ na nje YA NCHI
  yeremia enock from CHANIKAAmbwene : Aaah napenda kuimba live, lakini pia sijizuii kuimba kwa playback inategemea na mazingira ninayokuwepo, kwa Mito ya baraka mwimbaji aliyejiandaa nakufanya zoezi la kuimba live aliykuwa niyule mwimbaji aliyekuwa akizindua lakini mara nyingi ninapokuta live na nikaona nimefanya zoezi la kufanya live huwa ninafanya bila shaka, aah kuhusu ninaposali nilishasema, lakini kuhusu upole, upole ni tunda moja la Roho kama kuna mtu analiona tunda la Roho ndani yangu basi sifa kubwa ni kwamba Roho Mtakatifu ndio anayekuwa source wa hili tunda la roho kama lipo tunamshukuru Mungu na tuzidi kuombeana lisipotee, kiukweli mimi huwa napenda kusikiliza waimbaji tofauti tofauti naa madamu mwimbaji anaimba neno la Mungu ndani yake napenda kumsikiliza kwahiyo siwezi kuclarify nampenda zaidi mtu fulani kuliko mwingine no napenda kusikiliza muziki wa injili kama ulivyo wa ndani na nje uwe wa band au wa solo artist au wakwaya napenda kusikiliza kwahiyo sipendi kuweka wazi yupi nampenda nawapenda watu wote.

Ambwene :Nafikiri tumeshalijibu ni album tatu.
Ambwene : ha ha ha (kicheko) Ambwene bado anasoma Mbeya hajamaliza, yule dada ni mke wa mtu sio mke wake. • Rose Joel Mi nakukubali sana kihuduma, pia nadhani una kitu cha ziada ndani yako ambacho ni very special kihuduma naomba uendelee kuwa magotini zaidi ili Mungu alitimize kusudi lake ndani yako. unaitumiaje huduma ulionayo kusaidia wahitaji kama wajane na yatima? BARIKIWA!

Ambwene : Nilishalijibu pia. • Robert Nkyalu mi sina swali bali napenda kumjuza yeye ni moja ya waimbai nao wapenda sana hususani tabia yake ktk huduma hii imejaa sifa njema

Ambwene : Aminaa naomba tuzidi kuombeana.


 • Elda Philip kaka nakukubali sana yaani wew nimuimbaji nikisikiliza nyimbo zako nafalijika sana mungu akuzidishe ukubalike kila kona ya dunia

Ambwene : AMINA AMINA.


 • Steven Licheula DAA!!! NIMELUDI TENA,AMBWENE HUDUMA YAKO KWANINI USIIFANYE MASHULENI ILI UNYENYEKEVU WAKO UWAAMBUKIZE NAAMINI HATA KUFERI HAKUTOKWEPO.HEBU IMBA KIDOGO LIVE.

Ambwene :  ha ha ha (kicheko) aah huduma nimekuwa nikifanya mahali pote naamini shuleni nimekuwa nikifanya huduma mara nyingi, vyuo mbalimbali kwahiyo naamini hata shuleni ninafanya kwahiyo utaona....(haijasikika vizuri)  utaona ni kazi ya Roho Mtakatifu anaitenda vizuri( Silas (anaomba pia umuimbe japo kidogo live) okay ....nawewe unaniruhusu sasa (Silas : yeah), " Kama nikiwapenda wao wapendwaoo mwafanya ziada ganiii, wapendeni waombeeni wale wanaowaudhi Baba yenu Mbinguni atawapa thawabu, na watu watasema huu ndio upendo wa kweli" yeah nafikiri inatosha.

Silas Mbise : Asante sana Ambwene Mwasongwe, pia kwa niaba yake Ambwene Mwamwaja, Elie John The Philosopher  ikiwa ni timu nzima ya Gospel Kitaa, tunakushukuru kwa ushirikiano wako ulioutoa  kuweza kujibu maswali ambayo yameulizwa na wasikilizaji na wasomi pia wa Gospel Kitaa. Zaidi kama kuna mawasiliano yoyote pia kutoka kwako itakuwa ni vizuri tuweze kumpatia huyo msikilizaji wetu na msomaji wetu

Ambwene : Yeaa mawasiliano yapo lakini ningependa zaidi yatumike kwa ajili ya kihuduma zaidi kuliko matumizi mengine naatumia 0767 619 931 yeah

Silas Mbise : Ambwene mimi nikushukuru sana sana nisiongeze maswali mengi tutatafutana wakati mwingine ili tuweze kuongea nikutakie tu masomo mema na huduma njema kaka.

Ambwene : Amina Mungu awabariki sana na ninashukuru sana.


Kwa wiki hii, tumemalizana na Ambwene Mwasongwe, tukutane wiki ijayo Gospel Kitaa inavuka mipaka ambapo tutakuwa na mwimbaji nyota wa kwaya ya Ambassadors of Christ ya Rwanda Mrs Umulisa Yvonne Habimana ambaye amesolo wimbo wa "KWETU PAZURI", Je una swali lolote kwake kuhusu huduma yake na kwaya anayoimbia?

Uliza swali hapo chini sehemu ya maoni, ama kupitia barua pepe gospelkitaa@post.com na pia kupitia ukurasa wetu wa facebook. Barikiwa
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.