HABARI PICHA: DUNIANI KUNANI

Xiao Wei akiwa amebebwa na mama yake, ambapo madaktari wameeleza kuwa na hitilafu katika uti wake wa mgongo, jambo ambalo linahitaji uangalifu katika upasuaji, kwani hata wakiutaka ulipotokea, bado utatokea tena.

Askari wa kikosi cha uokoaji akiendelea na zoezi la kufukua na kuokoa watu na  pamoja na kuopoa miili iliyofunikw na kifusi cha jengo lenye ghorofa nne lilioanguka huko Mumbai, India na kuua takriban watu sita na majeruhi kadhaa mnamo Juni 22. ©AP
Nchini Canada, mafuriko yalipiga eneo la Alberta na kupelekea mto Alta kupwaa, matokeo yake ni taharuki mtaani, lakini kijana huyu na paka wake walisalimika kwa namna ya kipekee mara baada ya kutokea dirisha la nyuma ya gari lake na kuogelea mpaka sehemu salama. Picha za tukio hili ni kwa hisani ya Jordan Verlage wa The Canadian press Juni 21.


Msitu wa Black Forest Colorado, ambao umeungua na kuteketeza hekta na hekta za misitu Juni 13, lakini nyumba  hizi zikiwa hazijaathiriwa kati ya zaidi ya 360 zilizoteketea. Hii inaweza kutukumbusha kuwa muujiza wako uko palepale licha ya magumu ambayo yanaonekana kwenye jamii. ©Rick Wilking/Reuters
Vijana wa Kipalestina wakiwa kwenye kambi ya msimu wa kiangazi ambayo imeandaliwa na Islamic Jihad Movement, kipindi ambacho shule zimefungwa, kwenye mji wa Rafah, kusini mwa Gaza June 12. ©Said Khatib/AFP/Getty Images
Baada ya kutazam picha hizi na kufahamu kinachoendelea duniani, bado hujapata sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wanaokuzunguka, na kwa ajili ya tabasamu unaloamka nalo kila siku, ama hata kuona tatizo lako ni dogo kiasi gani?

Basi na kama Neno lisemavyo, tumshukuru Mungu kwa maana ni mwema na anatuwazia yaliyo mema daima.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.