KUTANA NA MWANAMAMA ALIYEIFIKISHA MAHAKAMANI BRITISH AIRWAYS BAADA YA KUKATAZWA KUVAA MSALABA

Mwanamama Nadia Eweida. Picha kwahisani ya The Gurdian UK.
Kama kuna watu ambao wanapigania imani kwa Mungu wao basi mmoja wao ni mwanadada Nadia Eweida mfanyakazi wa shirika la ndege Uingereza (BA), mwanadada huyu amepambana na shirika hilo kwa miaka sita ili apewe haki ya kuvaa msalaba ambao amekuwa akiuvaa shingoni kinyume na kanuni na sheria za wafanyakazi wa shirika hilo.

Mwanadada huyu alikataa kuvua cheni yake yenye msalaba mdogo ambayo amekuwa akivaa kila siku, licha ya mahakama kuu pamoja na mahakama ya rufaa kutolea nje kusikiliza kesi yake mwanadada huyo aliamua kuipeleka katika mahakama ya haki za binadamu ya bara ulaya ambayo inadaiwa kuwa na maamuzi magumu miaka ya karibuni lakini Nadia ameibuka mshindi katika kesi hiyo, ikitambua kama mwanadada huyo kubaguliwa kazini dhidi ya imani yake, ambapo mahakama hiyo imesema kitendo cha mwanadada huyo kunyimwa haki ya kuvaa msalaba wake inaonyesha ukiukwaji wa haki yake juu ya imani yake jambo ambalo yawezekana limepelekea kumchanganya, dhiki na wasiwasi 

TATIZO LILIVYOTOKEA.

Mwanadada Nadia ambaye ni mwajiriwa wa British Airways kama mtoa huduma kwa wateja(customer care) aliajiliwa mwezi May 1999 na kukatazwa kuvaa cheni yake ya msalaba kazini, kisha kupewa adhabu ya kutolipwa toka September 2006 mpaka February 2007. Mwanadada huyo amesema alipofika kuripoti kazini aliambiwa kuvua cheni yake mbele ya wafanyakazi wenzake ambao kuna wanaoamini na wasioamini juu ya Mungu kwakuwa ni marufuku kuvaa cheni yeyote unapokuwa kwenye vazi la kazi la kampuni hiyo, anasema aliwaambia kwamba yeye ni Mkristo na cheni yake ya msalaba aliyovaa inawakilisha imani yake lakini meneja wake wa zamu akamwambia kwamba endapo asingevua cheni hiyo alikuwa na mamlaka ya kumrudisha nyumbani muda huo bila malipo, Nadia amesema alijisikia vibaya sana kuambiwa vile alihisi kama kudhalilishwa kwakuwa meneja wake alirudia maneno hayo zaidi ya mara moja mbele ya wafanyakazi wengine ambao pia walifika kazini na viashiria vya imani zao jambo ambalo anasema hakuelewa kwanini ilikuwa kwake kwakuwa msalaba aliokuwa amevaa haukuwa wa dhahabu au kito cha thamani bali ni alama ya Ukristo.

"Nimefanya kazi na makampuni mengi ya ndege ya kimataifa toka mwaka 1970 lakini sijawahi kukutana na mambo kama haya ya kuzuiliwa kuvaa msalaba wangu, hakuna abiria, mfanyakazi au bosi wangu aliyenitaka nivue msalaba wangu". Nadia aliendelea kuwepo kazini baada ya askofu mkuu mstaafu wa Canterbury kanisa Anglican Rowan Williams kutishia kuuza moja ya kanisa kwa Paundi millioni 6.6 kama hisa kwa shirika hilo la ndege endapo mwanamama huyo ataondolewa kazini lakini kama haitoshi akapata watu wengi nyuma yake wakiwemo wanasiasa, makanisa na watu wa imani zingine wakisapoti uamuzi wa mwanamama huyo.

"Nimepitia wakati mgumu sana, mashaka, lakini nimekuwa na watu wengi wakunitia moyo na kunisaidia ikiwemo kulipa kodi ya nyumba na madeni mengine, ninashukuru sana makanisa na makundi ya Kikristo pamoja na kundi la haki za binadamu la Liberty(Liberty human rights organisation) ambao wamenilipia gharama yote ya kesi baada ya kushindwa na BA mahakama kuu, haikuwa jambo rahisi lakini imebidi kung'ang'ania ahadi za Mungu pia kuwa na imani na kumwamini yeye pekee, namwangalia Yesu pekee, kufunga na kuomba" amesema Nadia


Nadia ameongeza kwamba " kama haitoshi ili kunifanya nijisikie vibaya BA waliamua kunipa kazi sehemu ambayo hata nikivaa msalaba wangu wateja hawataweza kuniona, nilikataa siwezi kumkana Yesu kwasababu imeandikwa kwenye Biblia mtu yeyote atakayenikiri mbele za watu nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni,bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni"

Nadia amesema amepitia manyanyaso mengi wakati wote tangu kuanza kwa sakata hilo, ikiwemo maswali ya kumkatisha tamaa mda mwingine aliulidhwa maswali ya kukera nakufikia hali ya kuhamaki lakini imani yake ikamsaidia kupiga hatua mbele, alipojisikia mnyonge, mchungaji wake alimtia moyo na kusema kwamba msalaba aliokuwa anauvaa nikuashiria ameng'ang'ana kwa Yesu. Nadia hakuwa akipigania kwa nafsi yake pekee bali uamuzi uliotolewa na mahakama ya Ulaya ni kuonyesha Wakristo wote barani humo wana uhuru wa kuonyesha imani zao kwakuvaa alama za imani zao sehemu za kazi bila hofu ya chochote.

Source- Good Newspaper
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.