MWINJILISTI AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI MBAYA YA GARI MANEROMANGO

Askofu mkuu wa Lutheran na dayosisi ya mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa mwenye kofia akiwa na baadhi ya wachungaji na watumishi katika moja ya matukio ya dayosisi hiyo.
Ajali mbaya ya gari iliyotokea alhamisi iliyopita huko Maneromango mkoani Pwani imesababisha kifo cha mwinjilisti Charles Mboma wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini dayosisi ya mashariki na Pwani ambaye alifariki dunia papo hapo baada ya kutokea kwa ajali hiyo akiwa ndani ya gari aina ya Prado pamoja na watumishi wengine wa kanisa hilo wakielekea huko Maneromango kwenye kipindi cha Bible study kwa watumishi wa Dayosisi hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii ni kwamba mwinjilisti huyo alikuwa amekaa siti ya nyuma na kwamba ajali ilitokea kwenye moja ya kona mbaya zilizopo katika barabara hiyo, hivyo kufanya gari hilo lililokuwa na mchungaji,mwinjilisti,mratibu wa elimu ya Kikristo na mfanyakazi wote wa ushirika wa Mwenge lilipinduka zaidi ya mara mbili na marehemu kutupwa nje ya kioo na gari kumlalia wakati likipinduka, ambapo alikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe ambako hata hivyo jibu walilolipata ni kwamba mwinjilisti huyo alikwisha aga dunia.

Marehemu huyo ambaye aliingizwa kazini takribani miezi minne iliyopita akipewa kutunza mtaa wa Kiwangwa uliochini ya usharika wa Bagamoyo, alimaliza masomo yake ya Uinjilisti huko Usangi mwaka jana na kwamba ameacha mjane na mtoto wa miezi miwili. Ibada ya kuaga mwili wake ilifanyika jana katika usharika wa Mwenge kisha kusafirishwa kwenda mkoani Tanga kwa mazishi. BWANA alitoa na BWANA ametwaa jina la BWANA libarikiwe.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.