Hatimaye Mmasai wa WAPO Radio FM Stelius Sane ametangaza nia ya kuachana na ukapera baada ya kumvalisha pete ya uchumba binti anayetarajia kuwa mkewe mapema mwezi November mwaka huu jijini Dar es salaam katika ibada iliyofanyika katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Mabibo Sahara inayoongozwa na Askofu Geofrey Massawe.

Kutangaza nia kwa Stelius ambaye ni mtangazaji wa radio hiyo hususani kipindi cha Ipo njia cha usiku kumewaacha midomo wazi makapera wengine waliojazana ndani ya kituo hicho wakiongozwa na Silas Mbise, Anthony Joseph, Elie John na wengineo wakishindwa kuamini namna kijana mwenzao alivyowazidi kete mwe!


Comments/disqusion
No comments