'A NEW DAY' KUANZIA SAA KUMI WORD ALIVE


I need you to Reign, yaani nahitaji utawale ndio video itakayoambatana na uzinduzi wa albamu ya New Day Jumapili ya leo, 28 Septemba - kutoka kwa mwanadada Angel Bernard, kuanzia saa kumi jioni Word Alive Center, Sinza jijini Dar es Salaam.

Angel Bernard ambaye atasindikizwa na waimbaji lukuki ikiwemo Voice of Triumph kutoka Arusha, ni mwanadada mwenye sauti na kipaji cha kipekee, hasa kutokana na utunzi wa nyimbo zake unaohusisha pia lugha ya Kiingereza, kwa lugha ya wenzetu, tunaweza kusema, Contemporary Gospel Music.

Saa kumi kamili na kuendelea ni muda muafaka wa kujumuika na Angel kwenye ibada hii ambapo sifa na utukufu zitamrudia yeye aketiye enzini pake, BWANA Mungu. Njoo tujumuike pamoja, Gospel Kitaa itakuwepo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.