ANGEL BERNARD AFUNGA KAZI WORD ALIVE CENTER, PICHA 10 ZA AWALI

"Anajua sana, Yupo vizuri sana, Huyu ni level nyingine, I love you" hayo nibaadhi ya maneno ambayo GK imefanikiwa kuyasikia kutoka kwa watu ambao wameudhuria uzinduzi wa albam ya kwakwe Angel Bernard iitwayo A NEW DAY ambapo yeye mwenyewe alikuwa akiinua mkono juu na kuonyesha kido juu akimaanisha si yeye bali ni MUNGU.. Si ajabu hapo kuna mtu alijisemea moyoni, "Yaani binti yangu ni lazima nimpe jina la Angel".

Mchungaji Deo Lubala akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi kazi ya Angel
Katika uzinduzi huo ambao umefanyika Word Alive Center Sinza Mori ulienda sambamba na kutambulishwa na kuuza video ya wimbo wa NEED YOU TO REIGN ambayo video hiyo ya wimbo mmoja imegharimu sh milioni tano na na kutengenezwa Jijini Nairobi, Kenya.


 Kwa sasa tazama picha kumi za awali katika uzinduzi huo picha zaidi zitakujia.Angel Akiimba huku akiwa amejaa tabasamu


Voice of Triumph, kutoka Arusha

Bomby Johnson akimtukuza Mungu
Watu wakichezakwa Yesu
Mwandesha shughuli Fred Msungu
Mchungaji Deo Lubala wa Word Alive Center, Sinza Mori
Na mara baada ya tukio hilo, Angel alidhihirisha kuwa mtu mwenye hisia mchanganyiko, akishindwa la kufanya, aruke, alie, acheke, aombe, aimbe na mengine mengi. Kiufupi, akawashukuru wote waliofika kumsapoti.

https://www.facebook.com/angel.bernard.98
Hizo ni picha kumi za mwanzo kukupa ladha ya kile kilichofanyika katika uzinduzi wa albam ya kwakwe Angel Bernard. Endelea kuwa karibui na GK picha zaidi zinakujia.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.