BAADA YA KULA NYASI SASA WAUMINI WAANZA KUNYWESHWA PETROLI

Kiongozi mkuu wa Rabboni Ministries, Lesego Daniel
Wakati kitendo cha kuwaambia waumini wake kula majani (soma hapa) pamoja na kusimama juu yao huku akiwafanyia maombi  bado vikiwa vimewapiga butwaa watu wengi duniani, nabii Lesego Daniel wa huduma ya Rabboni Ministries iliyopo nchini Afrika ya kusini, sasa anawanywesha waumini wake mafuta ya petroli ambayo anadai ameyaombea na kugeuka kuwa juisi ya mananasi.

Katika video iliyopo chini utaweza kujionea kwa kina namna waumini wanavyogombea kunywa petroli (kama inavyosemekana) na kutoa shuhuda kwamba ina ladha nzuri kama juisi ya mananasi huku wengine wakimuomba nabii na profesa Lesego Daniel awaongeze juisi hiyo.

Ningependa kusikia ushuhuda wa huyu dada baada ya mchungaji kutua mgongoni na moka zake mwe.
Mafuta ya petrol kama ijulikanavyo kwamba ni hatari kwa afya ya binadamu kwani yanaweza kusababisha kupoteza uwezo wa kuona, kusababisha kizunguzungu, na hata mwili kudhoofika… 

Angalia video hii chini kuanzia dakika ya 5 na sekunde 40 (05:40) ili kujionea yanayojiri katika huduma ya nabii Lesego ambayo imejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi yake ya Afrika ya Kusini.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.