ISIS WATUMIA 'VIDEO GAME' NA AHADI YA WANAWAKE KWA VIJANA WAJIUNGE

Baadhi ya wanakikundi wa ISIS wakifurahia mmabaki ya ndege ya kivita ya Syria ambayo ilianguka ©Reuters/Stringer
Kundi la kigaidi lenye mrengo wa kutawala dini ya kiislamu na hatimaye kuwa na dola kubwa duniani, ISIS (Islamic State of Iraq & Syria) wameanza kampeni mpya ya kuwahamasisha vijana kujiunga na kundi hilo, kwa kutumia michezo ya video, ama kwa jina maarufu la Video Games.

Kundi hilo limefikia hatu ahiyo ikiwa ni siku kadhaa zimepita tokea kupatikana kwa barua yaoambayo walikuwa wakiisambaza kwa vijana kuwapa hamasa ya kujiunga na kundi hilo ili kufanya mashambulizi kwa 'wabaya' wao, kwa ahadi ya kulipwa fadhila ya wanawake mabikira 72, kipindi ambapo wawapo akhera, baada ya kupigana vita vitakatifu, na kwamba kila atakayefia kwenye uwanja wa via, ataitwa shujaa mtakatifu.

Kundi hili ambalo halina huruma kwa mtu ambaye yuko kinyume nao, awe mkristo ama muislamu mwenzao, kwa sasa limeanza kuwekeza kwenye michezo ambayo vijana wengi wa kiume hucheza, wakitumia ama computer au Playstation, na katika michezo hiyo, una mmoja maarufu uitwao Grand Theft Auto.

Grand Theft Auto ni mchezo wa video (video game) ambapo mtu humchezesha mhusika kwenye runinga na kufanya kile atakacho, ikiwemo kupora magari, kushambulia watu na kuwaibia pesa na mengineyo mengi yanayofanania, ili mradi tu mtu afurahi mwenyewe kwa vitendo vyake. Na katika toleo la kigaidi ambalo wanachukulia mfano huku, imepangwa kuwa kila atakayecheza, basi mchezo huo umhamasishe kujiunga na kikundi hicho kwa ajili ya hatua zaidi kikweli kweli.

Hadi sasa kundi hilo limeshatengeneza 'trailer' ambazo zinawaonyesha waklifurahia mashambulizi ambayo wanafanya, ikiwemo kwa video ambazo zinaonyesha wadunguaji wao wakishambulia kambo pinzani kwao, na kisha kufurahia kwa kusema, 'Allahu Akbar', yaani mungu mkubwa.

Haijafamaika kitengo cha habari cha chombo hicho kitaitumiaje michezo hiyo ipendwayo na vijana ulimwenguni kote, na pia hadi sasa haijajulikana kama watakuwa na toleo lao lini, kulingana na ratiba zao za mashambulizi.

Hivi karibuni Rais Obama alinuia kufanya mashambulizi kwa kikosi hicho, lakini akiondoa wazo kwa watu kwamba atapeleka majeshi ya ardhini, na kwa upande wake taifa la Ufaransa limeungana na Marekani, lakini wao wakishambulia kwa anga na ndege zao za Rafael, kwenye taifa la Iraq, maeneo ambayo mkikundi hicho kinahisiwa kuwa.

Zaidi ya wananchi 60,000 jamii ya kikurdi walihamia Uturuki kutoka Syria ndani ya masaa 24. ©Reuters/Stringer
Hadi kufikia wikiendi hii takribani watu sabini elfu wamekimbia makazi yao nchini Syria na kukimbilia Uturuki, ambako wanaamini watakuwa salama zaidi. Na katika hatua nyingine wapiganaji wa jamii ya kikurdi kutoka Uturuki na Iraq wameungana pamoja ili kuzuia mashambulizi yatakayotokana na kundi hilo linaloogopwa kutokana na dhamira yao. Gospel Kitaa itakuletea simulizi ya askari aliyesalimika kuuawa na kikundi hicho kati ya wenzake wengi tu na kufanikiwa kutoroka.


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.