KUTOKA MAKANISANI: MKESHA WA KUSIFU NA KUABUDU BCIC

Mwendesha Shughuli, MC King Chavala
Wiki hii kutoka makanisani tuko BCIC Mbezi Beach, ambako kumekuwepo mkesha mkubwa wa kusifu na kuabudu, ukihusisha pia maombi ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Ibada hiyo ambayo iliongozwa na Askofu Sylvester Gamanywa, ilikuwa na jumuiko la vijana kutoka kila kona ya jiji la Dar es Salaam, ambao pamoja na mengineyo mengi, walionyesha ujuzi wao kwenye sanaa.

Zifuatazo ni picha za matukio kama yalivyokuwa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, tarehe 28 Septemba 2014.
Rika zote zilikuwepo
Timu ya kusifu na kuabudu inayoshirikisha vijana kutoka vyuoni
Twende namna hii
'Nasi tumeweza pia kwenda namna hiyo' ni kama vile vijana hawa wanasema hivyo
Kila mtu kivyake vyake, ilimradi shangwe

Enhe... Askofu Sylvester Gamanywa na MC King Chavala
Pamoja na kiupepo cha usiku, jasho lilitoka watu hapa
Wasaa wa NENO
Ameeeeen
MaombiHakuna wa kupinga kwamba Yesu ni BWANA.Iwapo una tukio ambalo limejiri kanisani kwako, basi usisite kututumia picha na maelezo kwenye barua pepe yetu, gospelkitaa@post.com

Tukutane wiki ijayo, ambayo itakuwa mwezi Oktoba.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.