KWA TAARIFA YAKO: ALBUM ILIYOFANYA KWAYA ZIANZE KUIMBA KWA KUTUMIA CD (PLAYBACK)

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka maoni yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.


Joshua enzi hizo akiwa na wenzake wa Upendo Group kabla hajatoka na mkewe
KWA TAARIFA YAKO hii leo ni kukujulisha kuhusu album iliyoshawishi kwaya na makundi mengine nchini kuanza kuimba kwakutumia CD na kuachana na uimbaji wa live. Katika album hiyo tutazungumzia zaidi kuhusu moja ya wimbo ama pambio maarufu lililotamba sana na kuleta ushawishi mkubwa wa kuimbia CD kwa waimbaji nchini. waimbaji wakiwa ni kundi la Kijitonyama Upendo Group ambao walikuwa na a.k.a yao wakiitwa Spiritual voice, kundi hili ambalo limefanikiwa kutoa album mbalimbali zilizopendwa sana hasa album yao ya kwanza iitwayo 'Mungu Anakupenda', hata hivyo GK hatukujulishi kuhusu album hii bali album yao ya pili

KWA TAARIFA YAKO album yao ya pili iliyobeba jina la 'Bam bam' likiwa na nyimbo ama mapambio zaidi kama mambo sawasawa lakini wimbo uliobeba album hiyo uitwao Bam bam ama Haleluya ndio GK imeona ikuambie kama hujui kwamba, namna Upendo walivyokuwa wakishambulia jukwaa ulivutia wengi na kuachana na live na kuhamia kwenye cd. Ila wimbo wenyewe KWA TAARIFA YAKO kama hujui ni kwamba sauti yake imechukuliwa kutoka wimbo uitwao taste & pass wa kundi maarufu la zamani la Afrika ya kusini liitwalo Platform One kundi ambalo kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam watakumbuka radio Tumaini ilikuwa ikitumia sana miziki ya kundi hili majira ya asubuhi. 
KWA TAARIFA YAKO Upendo group walichukua sauti ya wimbo wote kama ulivyo na kuweka maneno yao, lakini kabla ya Upendo kuimba wimbo huu, walikuwa wanaimba ndani ya kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ambako walikuwa waimbaji wa kwaya hiyo. Kijitonyama Uinjilisti hawakurekodi bali huutumia kama wimbo wa jiving pamoja na nyimbo nyingine ambazo wamechukua sauti kutoka katika kundi hilo la Platform.(Pia kumbuka sio Kijitonyama tu bali pia makundi mbalimbali nchini walichukua mziki wa kundi hili na kuweka maneno yao).
KWA TAARIFA YAKO baada ya Upendo Group kujiondo kwenye kwaya hiyo ya Kijitonyama ndipo walipoboresha wimbo huo na kuurekodi katika album yao ya pili, kama ukikumbuka vyema katika KWA TAARIFA YAKO iliyotufungulia kipengele hiki tulizungumzia suala la Upendo group na kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama (kama hukusoma bonyeza HAPA) album yao ya kwanza ya Mungu Anakupenda walirekodi wakiwa bado ni wanakwaya wa Uinjilisti Kijitonyama.

KWA TAARIFA YAKO GK inaweza kuthubutu kwamba kundi hili ndilo lililochangia kwakiasi kikubwa watu kuacha kuimba live hususani kwaya za makanisani hasa kutokana na Upendo group walivyokuwa wakicheza kwa nguvu na watu wakiwashangilia sana hali iliyofanya kwaya ama vikundi vingi kujisahau wakidhani uimbaji wa kundi hilo ndio ulikuwa wakisasa zaidi kutokana na makofi na vigelegele vya wauimini wao kila Upendo group walipokuwa wakialikwa kutoa huduma kwenye sharika zao na kusahau kwamba walikuwa wanaua vipaji vyao kwani waumini hawajui hayo masuala ya live ama cd. Hata hivo Upendo group waliacha tabia ya kuimbia cd lakini waliofuata upepo mpaka leo bado wanaendelea nao.
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.