KWA TAARIFA YAKO: MWIMBAJI WA INJILI NCHINI ASIYETAJWA MIDOMONI KWA UBAYA

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka maoni yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.

KWA TAARIFA YAKO mdau wa GK kwa leo ni kuhusu mwimbaji wa siku nyingi nchini ambaye
alianza kutamba hususani jijini Dar es salaam kupitia kipindi maarufu cha muziki na nyimbo za dini cha radio Tumaini miaka ya 90s, akitamba na album yake ya kwanza iliyofahamika kwa jina la Nini? huyu si mwingine bali ni Jennifer Mgendi ambaye ni mke wa mtu pia ni mwigizaji na muandaaji wa filamu zenye kuelemisha jamii.

KWA TAARIFA YAKO licha ya kwamba mwanadada huyu kuwa wa kwanza kati ya waimbaji walioanza kutoa nyimbo zao binafsi miaka hiyo ya 90s na mpaka sasa bado akingali akimsifu Mungu wake, pia ni mmoja kati ya waimbaji ambao historia ya maisha yake imefanyika baraka kwa watu wengi kutokana na kutoandamwa na kashfa ama habari za kumsulubisha Kristo kwa mara ya pili msalabani. 

KWA TAARIFA YAKO Jennifer amekuwa akipendwa sana licha ya kwamba hana umaarufu kama waimbaji wengine ambao wanafahamika zaidi ndani na nje ya nchi lakini bado anakamata sifa za kutokuwepo tetesi za watu kuambiana iwe kwa suala la kutoza pesa kubwa akialikwa kwenye huduma ama tetesi nyingine ambazo zimekuwa zikiwakumbuka waimbaji wengine ziwe za kweli ama uongo lakini tetesi ambayo nimewahi kuisikia kutoka kwa mwimbaji huyu inadaiwa kwamba alikuwa kichwa darasani mpaka anamaliza elimu yake ya sekondari na chuo sifa hiyo ikingali ikiambatana naye.

KWA TAARIFA YAKO Jennifer ameelezea historia yake "Nilizaliwa tarehe 02 May, 1972 hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam, mama yangu akiwa Mwendapelu Nalaila na baba akiwa Fanuel Mgendi. Ninao ndugu watatu tuliozaliwa kwa baba ambao ni Mao Mgendi, Mlenge Mgendi na Noel Mgendi. Nimepata elimu yangu katika shule na vyuo mbalimbali kama shule ya msingi Mgulani,Shule ya sekondari Kisutu,Chuo cha Ualimu Korogwe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia nilifanya kazi katika taasisi mbalimbali zikiwemo Shule ya Sekondari Handeni, Shule ya Sekondari Tambaza, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Chuo Kikuu cha afya Muhimbili. Kuanzia 2007 niliacha kazi za kuajiriwa na kijiajiri katika kazi za sanaa na Muziki wa Injili". Mtembelee kwenye tovuti yake kwa kubonyeza HAPAKWA TAARIFA YAKO mwimbaji huyu ambaye GK inaweza kuthubutu kwamba anaurafiki wa karibu na Bahati Bukuku kutokana na kushirikishana kwenye baadhi ya kazi za uimbaji na pia kusaidiana katika huduma huwa anatulia kwa kipindi kirefu kabla ya kutoa album mpya kwa kustukiza na kuwakumbusha watu kwamba mtumishi Jennifer Mgendi bado yupo katika kumsifu Mungu. GK inazidi kumuombea mwana mama huyu katika huduma yake, Mungu azidi kumwinua kutoka utukufu hadi utukufu.Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO vinginevyo tukutane wiki ijayo...
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.