MAMBO YANAYOWEZA KUKUFANYA USIPATE MAVUNO


1.Mbegu mbovu

2. Ardhi isiyo na rutuba

3.Kukosea majira ya kupanda na kuvuna

4.Uhaba wa mvua katika msimu husika

5. Uwepo wa wanyama au wadudu wanaokula/ kuharibu mbegu uliyopanda

Mwalimu Dickson Kabigumila.


SABABU HIZI ZINAFANYA KAZI PIA KWENYE MASWALA YA UTOAJI NA SADAKA!

Mbegu mbovu: Kutoa sadaka iliyo kilema, isiyo sawa na maelekezo uliyowekewa moyoni na Mungu.

Ardhi isiyo na rutuba: Kutoa sadaka mahali ambapo "PANA JINA LA KUWA HAI LAKINI PAMEKUFA" Au Kutoa sadaka mahali ambapo "PANA KITI CHA ENZI CHA SHETANI"

Kukosea majira ya kupanda: Kuchelewa kuiwasilisha sadaka uliyoagizwa na Mungu kiasi kwamba unaipeleka wakati tayari KAZI NA MATUMIZI YAKE YAMEPITA. Mfano: Sadaka kwa ajili ya SEMINA AU MKUTANO WA INJILI halafu wewe unaileta BAADA YA SEMINA/ MKUTANO kila kitu kimemalizika! "UTII ULIOCHELEWA NI SAWA NA KUTOTII"

Uhaba wa mvua katika msimu husika: Umetoa sadaka ndiyo, Imepokelewa na kuombewa [Kumwagiliwa] Lakini bado Mungu AKAGOMA KUIKUZA ILI IKUPE MAZAO YA HAKI YAKO!

Uwepo wa wanyama au wadudu wanaoshambulia mbegu ardhini: Uwepo wa dhambi: "Sadaka ya mtu mbaya ni CHUKIZO KWA BWANA" Sadaka iliyoletwa kwa shinikizo la wanadamu: SAULI ALINYANG'ANYWA UFALME KWA KULETA SADAKA KWA MAELEKEZO YA WANADAMU BADALA YA MUNGU. Kumbuka, "NI MBWEHA WADOGO WADOGO WANAOHARIBU MZABIBU [MATUNDA]"

Tafakari na ujipime Utoaji wako, 
Mwl D.C.K 
www.yesunibwana.org 
dicoka@rocketmail.com +255655 466 675


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.