MCHUNGAJI AFUNGWA KWA KURUHUSU SAUTI KUBWA KUTOKA KANISANI KWAKE

Mchungaji Johnnie Clark.©Islandpacket
Mchungaji Johnnie Clark wa kanisa la Rehoboth United Assemblies huko kusini mwa jimbo la Carolina nchini Marekani amepewa kifungo cha wiki mbili jela kwa kosa la kanisa lake kutoa sauti kubwa na kuleta kero kwa majirani na kanisa hilo.

Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha jimbo hilo WLTX TV Columbia kimesema, polisi imesema imekuwa ikiuita uongozi wa kanisa hilo zaidi ya mara 50 kwa kosa hilo la kelele ambalo limekuwa likilalamikiwa na majirani huku katika ripoti hiyo ikidaiwa asilimia kubwa ya malalamiko hayo yanatoka kwa jirani mmoja tu.

Kwa upande wa mke wa mchungaji huyo Harriet Clark amekiambia kituo hicho kwamba haamini
Mchungaji Johnnie na Herriet Clark katika picha.
kilichotokea kwa mumewe kufungwa kwa kosa la kumtumikia Mungu, baada ya hili nini kinafuata sasa? ni juu yao majirani kusema kama wanabugudhiwa na sauti ama la, alimalizia mchungaji Herriet.

Kutokana na tatizo hilo jaji ameamuru kanisa hilo kutotumia ngoma (drums), vipaza sauti kati ya saa 2 usiku na saa 2 asubuhi ikiwa ni adhabu ya miaka miwili. Kwa upande wa mmoja wa majirani na muumini wa kanisa hilo kijana Thomas Borders(20) amesema unaweza kuchukua mashine ya kukatia nyasi na kwenda nje kuifanyia kazi hata kama kuna mtu atalalamika lakini hakuna hatua itakayochukuliwa, lakini inapokuja suala la kumwabudu Mungu ni tatizo.

Viongozi wa kanisa hilo wamedai kanisa limekuwepo kwa muda mrefu katika enero hilo hata kabla ya kuwepo kwa nyumba za majirani hao na kwamba kanisa halitakiwa kuadhibiwa kwa ajili ya hilo. Njia kuu ya kutibu tatizo hilo ni kwa mchungaji Clark kuweka vifaa vya kuzuia sauti kutoka nje (sound proof) kitu ambacho hata hivyo si rahisi kwakuwa ni bei kubwa.
 
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.