MISTARI 7 YA BIBLIA IHUSUYO FURAHA

Furaha hutuhuisha upya. ©Gallery Hip
Kuwa na furaha mara zote, ama kuwa kwenye hali ya kufurahi huweza kutukumbusha enzi za utotoni. Wengi wetu hufurahi kupitia vitu ambavyo tunapenda kufanya mara kadhaa, mathalani kula, kukutana na marafiki, kusikilia muziki na hata kutazama sinema. Lakini furaha ya kweli hasa inapatikana kama sehemu ya tunda la roho.

Ifuatayo ni mistari 7 ihusuyo furaha, kama ambavyo John Calahan amezikusanya.

Kumbukumbu la Torati 16:15
Siku saba mfanyie sikukuu BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, atakubarikia katika maongeo yako yote, na katika kazi zote za mikono yako, nawe uwe katika kufurahi kabisa.

Nehemia 8:10
Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa BWANA wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.

Mhubiri 9:7
Wewe enenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako.

Isaya 9:3
Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao; Wanafurahi mbele zako, Kama furaha ya wakati wa mavuno, Kama wati wafurahivyo wagawanyapo nyara.

Zaburi 5:11-12
Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia. Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.

Isaya 12:6
Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.

1 Samweli 18:6
Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.