NCHI YA AHADI IPO LAKINI ILI UIMILIKI LAZIMA UPIGANE VITA NA KUSHINDA

NCHI YA AHADI IPO LAKINI ILI UIMILIKI LAZIMA UPIGANE VITA NA KUSHINDA:

Mathayo 11:12 inasema....
Tangu siku za Yohana mbatizaji hata sasa ufalme Wa Mbinguni hupatikana kwa Nguvu,nao wenye Nguvu wauteka;
Ndugu zangu kila Mungu alichokuaidi unaitaji kupigana ili umiliki kwa sababu adui hata ki wewe
umiliki,hakuna Mtu anaye taka kumiliki, akamili pasipo vita,iwe ni raisi au Mtu yeyote au sehemu yeyote uwezi kupata kitu na kukimiliki tu kirasi lazima uwe Mtu Wa vita,maana kile unachotaka kukimiliki kuna mtu hataki wewe ukimiliki au kile unachoitaji kuna mtu hataki ukipate,iwe ni ndoa kuna Mtu hataki hiyo ndoa yako isimame,iwe ni biashara kuna Mtu ambaye hataki uwe nayo au akiona ikiendelea,au kazi kuna Mtu ambaye hataki kuona una kazi au umefanikiwa katika kazi hiyo, au ni katika elimu kuna Mtu ambaye hataki kuona unaelimu au elimu yako inakusaidia,au nyumba kuna Mtu hataki kuona Kama unajenga kabisa,au Kama ni watoto kuna Mtu ambaye hataki kuona watoto wako wanaelimu au uwe na watoto,

Kumbuka tu kwamba adui hataki umiliki kitu chochote,na Kama hataki umiliki basi unaitaji kupigana ili umiliki,wana Wa Israel waliahidiwa nchi ya Kanaani,lakini ilikuwa lazima wapigane vita ili kuja kuimiliki haikuwa tu raisi kwa sababu wameahidiwa basi wamiliki ilikuwa lazima wapigane wamiliki,hata wewe iwe ni afya lazima upigane ili umiliki hakuna kitu utakacho taka kumiliki usipopigana,
Hesabu 13:17-18 inasema...
Musa akawapeleka ili waipeleleze nchi ya kanaani,akawambia pandeni sasa katika Negebu mkapande milimani,mkaitazame nchi ni ya namna gani;na watu wanaokaa ndani yake,kwamba ni wachache au wengi,unaona hapa nchi wamepewa lakini lazima wapigane ili waingie waimiliki,
Paul anasema hivi
1wakorintho 16:9 kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa Wa kufaa sana,na wako wengi wanipingao,

Kama uwezi kupigana hata ule mlango Wa mafanikio ambao Mungu amekufungulia uwezi kuupata,kuna ahadi nyingi sana Mungu ameahidi kwa watu lakini utashaanga hawajapokea kwa nini kwa sababu adui amezuia lakini kwa sababu wewe siyo Mtu Wa vita ili upokee,angalia Daniel alikuwa amefunga na kuomba lakini majibu yalikuja siku ile ya kwanza lakini adui aliyazuia siku ishirini na moja,mpaka malaika anakuja kumpigania majibu yake yapite,kuna vitu vyako vingi vimezuiliwa mpaka umepigana vinginevyo uwezi pokea au kupata,wokovu siyo lelemama,
Isaya 60:11-12 inasema hivi …

Malango yako nayo yatakuwa wazi daima;hayatafungwa mchana na usiku ili watu wapate kukuletea utajiri Wa Mataifa na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao,kwa maana kila taifa na ufalme Wa watu wasiyo taka kukutumikia wataangamia;Naam Mataifa hayo wataharibiwa kabisa.
Unaona Mungu alichokisema hapa malango yako yatakuwa wazi daima lakini paulo anasema kuwa wengi wanipingao maana yake wanaofunga,milango yako Kama imefungwa lazima uifunguwe na kufungua lazima upigane,kile utakavyomiliki ni vile utakavyo pigana,
Ili umiliki afya ambayo Yesu amekupa lazima umiliki kwa vita maana shetani anataka uwe na magonjwa,waefeso anasema vita vyetu si vya damu na nyama,maana yake tuna vita,maombi yangu kwako Leo katika Jina la Yesu ushinde kila unapopiga katika Jina la Yesu:Amen

Ujumbe kutoka kwa King Sam.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.