PAPA FRANCIS HATARINI DHIDI YA SHAMBULIZI LA KIGAIDI

Papa Francis akiwa kwenye gari lake, Pope mobile huku akisalimiana na umati uliojitokeza kumsalimu, kwenye picha ya mapema mwezi Aprili 2014. ©Tony Gentile/Reuters
Wakati dunia ikiwa inashangazwa na kundi jipya la kigaidi la ISIS (Islamic State of Iraq and Syria), linalotekeleza mauaji yake kwenye mataifa mbalimbali hasahasa Iraq na Syria,likidai kutawala dini ya Kiislamu duninani kote, taarifa mpya zinaeleza kuwa kuna hofu ya kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, kushambuliwa.

Papa ambaye yuko kwenye mkakati wa kufanya ziara kwenye taifa la Albania mnamo wiki ijayo, anatarajiwa kuwa na wakati mgumu kwenye taifa hilo linalotambulika kama la Kiislamu, ambapo huenda kundi la ISIS likawepo.

Ziara hioy ambayo itachukua siku moja, imeelezwa na msemaji mkuu wa Vatican, Mtumishi Federico Lombardi kuwa, licha ya kwamba matukio yanayoendelea duniani ni ya kustua, hakuna haja ya kuwa na hofu kuhusu usalama wa Papa, na kwamba hawaoni haja ya kuchukua hatua zaidi za kumsafirisha Papa kwenye gari linalozuia risasi, badala ya gari lake la siku zote ambalo liko wazi.

Kwa upande wake, balozi wa taifa la Iraq huko Roma, amesema kuwa licha ya kwamba kundi la ISIS linaweza kudharauliwa, lakini lengo lake pia ni kummaliza Papa, ambaye ana ushawishi mkubwa duniani.

"Sote tunatambua kwamba kundi hili linalengo gani, lakini isiwe chanzo cha kuacha kufikiri kwamba wanaweza kumshambulia Papa." Balozi Habeeb Al Sadr amenukukliwa na gazeti la kila siku la II Mattino.

Wakati balozi akieleza hivyo, mnsemaji wa Vaticna alibaki kusisitiza kwamba hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, kwani hakuna tishio lolote ambalo limetolewa hadi sasa.

Papa Francis anatembelea Albania kutazamia kuanza upya kwa uwepo Wakristo kwenye taifa hilo, ambapo katika miaka ya nyuma, waamini wa dini hio waliuawa. Pamoja na hayo Papa ataeleza kuhusu umoja, ambapo Wakatoliki, Wa-orthodox na Waislamu walikuwa wakifanya kazi pamoja kulijenga taifa lao.

Papa John Paul II ndio kiongozi mkuu wa kwanza wa Kanisa Katoliki kutembelea Albania mwaka 1993, amb apo imeelezwauwa ujio wa Papa Francis, utahuisha ukatoliki nchini humo, ikiwemo kwa kuwasimika maaskofu wapya wanne.

Charisma imeandika
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.