SARAH SHILLA NA YAHWE LIVE RECORDING KATIKA PICHA

Sarah akiwa amezama kwenye kumuabudu Mungu.
Mwisho wa wiki kumekuwa na matukio mbalimbali jijini Dar es Salaam, ambapo Mungu amerudishiwa sifa na utukufu kupitia uimbaji. Na kati ya matukio hayo, lipo la live recording ambayo imefanywa naye mwanadada Sarah Shilla Ndosi kwenye ukumbi wa kanisa la Victory Christian Center Tabernacle (VCCT)

Tukio hilo la aina yake lilijiri kuanzia mida ya saa kumi jioni hadi saa mbili usiku, likishuhudia albamu ya YAHWE ikirekodiwa kwa ustadi mkubwa, huku pia ikiambatana na usakaji wa vipaji kwa waliohudhuria siku hiyo, zawadi kabambe zikitolewa.

Albamu hiyo ya Yahwe yenye nyimbo kumi inatarajiwa kuzinduliwa mwishoni wa mwezi Disemba ama mapema Januari, huku ikiwa imejaa zaidi nyimbo za kuabudu. Kama ulikosa tukio hilo, basi kaa chonjo kwa ajili ya uzinduzi.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo la mwanadada Sarah Shilla, ambaye pamoja na uinjilisti, pia ni fashion model.

Sarah pamoja na washindi wa shindano la vipaji vya kuimba. Mshindi wa kwanza amepewa fursa ya kurekodi wimbo, wa pili akipelekwa shule ya muziki, na wa tatu akipata fursa ya kuimba popote pale ambapo Paul Clement, Sarah Shilla Ndosi ama Bomby Johnson watakuwa wakihudumu.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.