SERIKALI YAWAPIGA MARUFUKU WANANCHI WAKE KWENDA KWA TB JOSHUA NIGERIA

Kanisa la Mtume TB Joshua kabla ya kuanguka.
Wakati vyombo vya habari vya kimataifa vikiripoti watu 115 wamefariki dunia kutokana na kuanguka kwa kanisa la mtume TB Joshua wa Nigeria la Church of All Nations, serikali ya Cameroon imewapiga marufuku wananchi wake kwenda kanisani au kujihusisha na mtume huyo ikidai kwamba ni wakala wa shetani na kwamba amekuwa akiudanganya umma kupitia miujiza waliyoiita ya kishetani.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa mambo ya nje na mahusiano wa Cameroon mheshimiwa Henri Eyebe Ayissi katika waraka wake alioutoa mapema wiki iliyopita ukiwa na kichwa cha habari kisemacho 'shetani yupo ndani ya nyumba' akimaanisha mtume TB Joshua kwa kumuita mtoto wa shetani akijofanya ni mtumishi wa Mungu.

Waziri huyo amewaonya mamia ya wananchi wa Cameroon wanaokwenda kusini magharibi mwa jiji
Waziri Henri Eyebe Ayissi 
la Lagos nchini Nigeria kwaajili ya miujiza kanisani kwa TB Joshua kuachana na safari hizo kwani matokeo yeyote watakayopata itakuwa juu yao wala nchi yao haitasimama kuwatetea. Waraka huo ambao umeandikwa kwa lugha ya kifaransa (Cameroon wanazungumza kifaransa) hapa ukiwa umetafsiriwa kwa kiingereza “The Ministry of Foreign Affairs warns those who by naivety or deception of Emmanuel TV’s captivating images, or even those who by hopelessness, envisage taking the pilgrimage to Pastor TB Joshua’s Synagogue Church Of All Nations in Lagos, that they will do so at their own risk". ameandika waziri hugo.

Aidha ameongeza kwamba hali ya wanaume na wanawake wa nchi hiyo kwenda kwa mtume Joshua ni tabia yao ya kupenda miujiza na wanapokuwa ndani ya kanisa hilo wanajikuta katika hali ya kudanganywa na kubaki kama wanyama. "wanawake wanabakwa na kunyang'anywa vitu vyao na wanyang'anyi na kuachwa wakilala mitaani bila msaada, matukio mengi ya mauaji yamerekodiwa na haya ni mbali na matukio ambayo hayajarekodiwa katika ubalozi wa Cameroon jijini Lagos kwasabau wahusika wanaona aibu kuyaeleza yaliyowakumba" amesema waziri huyo.

Waziri huyo akaenda mbele zaidi kwakusema wakati Biblia inasema kuwasaidia maskini, TB Joshua anaonekana kila leo akigawa mabegi ya mchele kwa watu wenye uhitaji. Wakati huohuo gazeti la Cameroon katika ripoti yake wiki iliyopita limeandika mamia ya wananchi wa nchi hiyo wamekuwa wakiuza mali zao zikiwemo nyumba, mashamba au kukopa pesa wakitarajia kupata miujiza kutoka kanisani kwa TB Joshua lakini wanaishia kukata tamaa wanapofika Lagos.

 
Mtume TB Joshua akikagua zoezi la uokoaji kanisani kwake.
Magazeti yameandika kwamba runinga ya mtume huyo imekuwa maarufu sana nchini Cameroon kwakutazamwa na waengi na kufanya wengi kupata majaribu ya kusafiri kwenda kwa mtume huyo ili kupata uponyaji ama baraka. Gazeti hilo limeandika kwamba kwasasa mtume huyo anatazamwa takribani kila nyumba nchini humo na kuamini miujiza yote wanayoiona kupitia runinga huku gazeti moja likimnukuu mmoja wa watu waliokwenda kwa mtume huyo na kurejea kwamba ameweza kuokoa ahadi yake na mtumishi huyo wa Kristo na kwamba pesa aliyotumia kiasi cha shilingi 150,000 za Cameroon (FCA) imekuwa ikiongezeka kutegemea na matibabu na hali ya mgonjwa, hali iliyosababisha kutoelewana kwa wananchi wa nchi hiyo na kufunga safari hadi kanisani kwa mtume huyo lakini matokeo yake wanageuka wakimbizi kwenye ubalozi wao uliopo Lagos.

Hii si mara ya kwanza kwa Cameroon kutoa tamko la kuwakataza wananchi wake kwenda nchini Nigeria kwa mtume huyo ambaye amekuwa akipata upinzani katika baadhi ya nchi barani Afrika ikiwemo Zimbabwe ambako kuna taarifa inasema nchi hiyo haitaruhusu mtume huyo kukanyaga ardhi yao ingawa kuna fununu kwamba mtume huyo anapanga kwenda katika nchi hiyo.

Chanzo 233live

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.