SOMA RASIMU YA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM

Sehemu ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya kundi la UKAWA kutoka nje
Habari kutoka Dodoma mdau wa GK, mjadala wa katiba mpya unaendelea kutoka bunge maalum, na mivutano pia ikiwemo - ndani na nje bunge hilo.

Ni hivi karibuni Jukwaa la Wakristo nchini limetoa tamko kutaka Bunge Maalum lisitishwe ili kupatikane kwanza muafaka (usome hapa) kwa ajili ya kuwa ukurasa mmoja kwenye kile kinachoendelea. Lakini pia kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi unaoundwa na vyama kama CHADEMA, CUF na NCCR Mageuzi nao wako nje wakishikilia msimamo wao wa kuipinga katiba, ambayo wanaiita ya Chama Cha Mapinduzi.

Na kwa upande wao Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA wako katika purukushani na jeshi la polisi kutokana na kutangaza maandamano nchi nzima kupinga kile kinachoelezwa kuwa ni katiba isiyoya wananchi ndio inatengenezwa bungeni kwa sasa.

Ifuatayo ni rasimu ya kwanza iliyopendekezwa na Bunge Maalum, kama ilivyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati ya uandishi ya Bunge Maalum, Mhe. Andrew Chenge. Nawe kama mwananchi, ni vema ukapitia na kutambua nini kimezungumzwa na ni fursa gani kwa taifa la Tanzania.


Gospel Kitaa imepiga kambi mjini Dodoma, na itakuhabarisha kila kinachojiri kwa kadri iwezekanavyo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.