SOMO: AKILI ILIYOROGWA - MCHUNGAJI GWAJIMAI: NENO LA MSINGI: Wagalatia 3:1
1 Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?
Kumbe Mtu anaweza kulogwa akili yake bila kujua.
Musa alipotaka kutengeneza hema ya kukutania Mungu alimwelekeza
Kutoka 35 
30 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, Bwana amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda;
31 naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina;
32 na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba,
33 na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za werevu kila aina.
34 Naye amemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani.
35 Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.
kwenye maandiko Matakatifu yanaonyesha kuwa akili zake hazichunguziki na watu waliookoka wanatakiwa watumie akili zao na maandiko yanasema Mungu ni Mungu mwenye nguvu msifuni kwaakili na uone jinsi alivyoteswa msalabani na leo Mungu afungue maisha yako na akili yako kuna baadhi ya majibu yako kwenye akili zako.
Wachawi wanatuonea wivu kwamba kuna baadhi ya majibu yapo kwenye akili zetu na ukiishi kwa kumtegea mtu utakufa masikini ndio maana Paulo anawaandikia wagalatia kwamba enyi wagalatia msio na akili ninani aliyewaloga? Akili zao zimetiwa giza
Waefeso 4
17 Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao;
18 ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;
19 ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani.
20 Bali ninyi, sivyo mlivyojifunza Kristo;

II: MUNGU ALIPOMUUMBA MTU ALIMUUMBA KWA VIPANDE VITATU
1. Roho
2. Mwlili
3. Nafsi ambapo kuna kitengo cha nia ambapo mtu anajaza elimu, pia kuna eneo la hisia na kuna eneo la utashi lakini kuna eneo la akili ndio maana unaweza kumkuta mtu kijijini amekaa hajasoma lakini anamafanikio makubwa.
Ndio maana farao aliwaita watu wenye akili, wachawi na waganga ili washindane na Musa nahii inatuonyesha kwamba kumbe wenye akili ni tofauti na wachawi na waganga. Kila mtu unayemwona amepewa akili na Mungu na mtu akitaka kukukomesha anatuma mashetani ya kufunga akili yako ndio wale watu wanaoshindwa kufanya jambo kwasababu akili zao zimefungwa. Akili ni jambo kubwa sana kwenye maisha yako na Mungu amekupa akili za kutosha mkeo, za kuitosha familia na ndipo ugombee uongozi.
Mungu wa dunia hii anauwezo wa kuifanya akili yako isifanye zaidi ya hapo ulipofikia, nebkadneza naye alikuwa anaita wenye akili, wachawi, na waganga sababu alikuwa anajua akili inaweza kutumika kama uchawi utashindwa. Mfano wewe umeumbwa na Mungu unaakili sana Mungu ameweka akili ndani yako na wachawi wanakutumia jini au pepo kuja kukaa ndani yako na unashindwa kuwaza hata ukiingia darasani huelewi na unaomba lakini akili yako imefungwa usielewe.
Zaburi 147
5 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka.
6 Bwana huwategemeza wenye upole, Huwaangusha chini wenye jeuri.
2Samweli 14: 2 Yoabu akatuma watu waende Tekoa, akaleta kutoka huko mwanamke mwenye akili, akamwambia, Nakusihi, ujifanye kama unakaa matanga, ukavae nguo za kufiwa, nakusihi, wala usijitie mafuta, ila ukafanane na mwanamke aliyeomboleza siku nyingi kwa ajili yake aliyefariki;
20 mtumwa wako Yoabu ameyatenda haya ili kubadili uso wa jambo hili; na bwana wangu anayo akili, kama akili ya malaika wa Mungu, hata ajue mambo yote ya duniani.
Anamwambia mfalme Daudi kwamba kuna jambo limefanyika lakini wewe unayo akili kama ya malaika wa Mungu, kumbe malaika nao wanaakili. Mfalme kabla hajafa akamwambia mwanangu umtendee kwa akili ili uweze kutawala vizuri. Siku moja Daudi akafariki na akamwacha mwanae Sulemani akijua kuna mtu wa kumtendea kwa akili, siku moja mfalme akamwambia yoabu nataka kuonana na wewe na yoabu akaogopa akidhani atauliwa na kwa desturi za wayahudi mtu ukitaka kumuua anakimbilia kushika pembe ya madhabahu ili akiuawa aliyemuua anakuwa amelaaniwa na yoabu akaenda kushika kwenye madhabahu ya Bwana na akasema nitafia hapahapa kwenye madhabahu ya bwana na mfalme akasema kwakuwa amesema atafia kwenye madhabahu basi muueni kama alivyosema. Sasa na wewe unatakiwa utumie akili kutenda
Ndio maana bwana yesu akasema mpende bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa akili yako yote kumbe hata Bwana anapendwa kwa akili zetu zote. Unamkuta mtu anaangalia televisheni kuanzia asubuhu mpaka jioni alafu analalamika serikali haiangalii watu wa chini kumbe yeye hatumii akili kufanya mambo. Ndio maana unakuta mahali watu wakianzisha biashara wanakuja na wengine wanafanya kama hiyo pembeni yao
Ndio maana kina shadrack, meshack, na Abednego walichukuliwa ili walishwe vizuri na kulelewa vizuri ili akili zao zitumike na jambo likitokea walikuwa wanafuatwa na kutoa ufafanuzi kwa akili zao, sasa basi unakuta mtu anakuona una akili na anaamua kuifunga akili yako na unamkuta mtu anakaa mahala pabaya ana Ng’ombe elfu tatu na usiku akilala ukiwa mita mia moja unakiona kitanda chake, na mwingine ukimuuliza unafanya kazi gani anakujibu kwa ujasiri mimi ni mama wa nyumbani.
Biblia inasema mwana wa Adamu amekuja naye ametupa akili. Unamkuta mtu hajaoa na anatimiza miaka 50 anasema anajipanga unajua huyu amelogwa. Kuna wachawi wanaochukua akili ya mtu na anaanza kuitumia na kwenye kichwa chake anabakiza mashetani ambayo yanamfanya anakuwa na laana na mikosi.

III: MTU ATASIFIWA KWA KADIRI YA AKILI ZAKE.
Mithali 12
8 Mtu atasifiwa kwa kadiri ya akili zake; Bali mwenye moyo wa ukaidi atadharauliwa.
Mtu anasifiwa kwa jinsi akili yake ilivyo na mchawi anakuja anachukua akili na anaondoka nayo na vile vitu unavyotaka kuvifanya unashindwa ni kutokana na akili ikiwa imechukuliwa unakuta mtu akianza kusoma kichwa kinauma au anasinzia kumbe ni watu wamechukua akili yake na wanaenda kuitumia mahali Fulani na unakuta mtu ni mgonjwa lakini akili inakuwa imechukuliwa inatumika mahali na wewe unakuwa unaona giza, maskio yanauma, unaona ukunguukungu na ndio maana watu wengine si lazima waombewe wapone ni kumrudishia akili yake. Unakuta mtu unamrudisha anasema nilikuwa Bungeni nyuma ya kiti cha spika lakini kimsingi ni kwamba akili yake ilikuwa inatumika ili kumfanya spika asiumbuke pindi anapoulizwa maswali ya ghafla na huyu mtu aliye ibiwa akili yake anabaki kuuza magazeti, kuwa ombaomba, anabaki mtu mzima lakini akili yake haipo wameichukua wanaitumia kisiasa kibiashara na mambo mengine.
Kama malaika wanaakili na sisi lazima tuwe na akili kama Mungu ana akili na akili zake hazichunguziki kwa nini sisi tusiwe na akili lazima akili zetu zirudi kwa jina la Yesu. Kujihatarisha sio hatari lakini kutokujihatariasha ni hatari kubwa kuliko zote, ili bihashara yeyote ianze lazima kuwe na uthubutu, na unamkuta mtu mgonjwa ana presha lakini watu wanatibu presha kumbe mtu huyu anaakili sana ili anapoangaika kutibu presha wanatumia akili yake
Kwa jina la Yesu ninakataa kwa jina la yesu mtu yeyote aliyechukua akili yangu akanifunga na magonjwa ninaamurui rudisha akili yangu kwa jina la Yesu akili ya biashara, akili ya kusimamia miradi, akili ya kujenga kanisa, akili za kusafiri kwa jina la Yesu, umenijia kwa uchawi nakujia kwa jina la Bwana wa majeshi akili njooo kwa jina la Yesu.
Mtu mwingine hajui anakwambia mchungaji wameniloga nisipendwe, nisisafiri, nisipate kazi lakini sio kwamba wamekuloga wamechukua akili na ndio maana kwenye filosofi wanasema angalia unachokisema sema kunasiku utakitenda uwe mwangalifu na unachokitenda kunasiku kitakuwa tabia na tabia ya mtu ndio asili ya mtu. Lakini unalalamika jamani wameniloga kumbe akili imechukuliwa hebu jiulize hapo ulipo unampango gani wa maendeleo una kuta hakuna, lakini kwa kawaida inatakiwa uanze kuplani na hiyo plani yako ndio itakayo kupa fedha lakini umelogwa akili yako inatumika mahali unatakiwa ukatae kwa jina la Yesu.
Akili yako inapolala ndio wale tunaowaita usingizi wa kiroho ingawa unaona lakini umelala usingizi na Yule aliyekuibia akili zako mnyanganye kwa jina la Yesu. sio wakati wa kushangilia ametajirika ni wakati wa kuwaza ameupata wapi utajiri ule , si wakati wa kuuliza ameshindaje uongozi ule ni wakati wa kuwaza ameupata wapi uongozi ule, sasa ni lazima turudishe akili zetu zote zilizoibiwa kwa jina la Yesu, ni wakati wa kuanza kuitumia akili yako ili kuinua familia yako,ni wakati wa kutumia akili tuliyopewa na Mungu kwa jina la Yesu
Kwa jina la Yesu wale waliotafuna akili yangu ninawaamuru watapike akili yangu kwa jina la Yesu . unakuta unawaza kwamba mimi ninaweza kufanya zaidi ya hapa ni kweli ila kuna mahali wameitafuna akili yako na wamekuloga ili waitumie mahali. Unakuta akili inatumika kuzaa watoto wa kijini baharini lakini akili hiyohiyo ingetumika kuwafanya watu waokoke na mtu huyu anachiwa magonjwa ndani yake. Wanapoiiba akili yako wanakuvisha akili ya uoga kumbe ile akili ya ujasiri inapoibiwa wanakuachiwa akili ya uoga na unatakiwa ukatae uoga ulionao sababu sio asili yako hiyo kwa jina la Yesu.
Akili yangu iliyofungiwa shimoni njoo kwa jina la Yesu, naishinda akili ya uoga kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu naamuru akili yangu njoo, akili ya biashara, akili ya ubunifu, akili ya fedha, na mtu yeyote anayetumia akili yangu naamuru achia akili yangu kwa jina la Yesu, akili ya kuanza biashara , akili ya kufanya kazi, akili ya kubuni njoo kwa jina la Yesu napokonya akili kwa jina la Yesu, nakunyanganya akili yangu kwa jina la Yesu uliyemeza akiliyangu nakutapisha kwa jina la Yesu ewe mkurugenzi uliyemeza masomo yangu nakutapisha kwa jina la Yesu, ewe uliyemeza akili yangu ya ubunifu nakunyanganya kwa kwa jina la Yesu, akili ya kusafiri, akili ya kuongea, akili ya kutenda njoo kwa jina la Yesu, akili iliyoko mapangoni, mashimoni, baharini njoo kwa jina la Yesu, akili ya miradi, akili ya kuanzisha makampuni, akili ya kumtumikia Mungu njoo kwa jina la Yesu, rudisha akili yangu kwa jina la Yesu, akili inayotumiwa na majini kutengeneza bacteria na virusi vya magonjwa nashindana nanyi kwa jina la Yesu, akili ya kubuni miradi akili ya kuita miradi, akili ya kuota kazi njooo kwa jina la Yesu, akili ya kujua cha kufanya , akili ya kujua cha kutenda njoo kwa jina la Yesu, ninaifungua akili yangu kwa jina la Yesu, ninawashambulia mashetani wote na wachawi wote mnaoishikiila akili yangu kwa jina la Yesu, akili yangu inayotumika mahala popote ninairudhisha kwa jina la Yesu naondoa akili za kishetani na magonjwa yote yaliyowekwa ndani yangu kwa jina la Yesu, vifungo vya akili ninavifungua kwa jina la Yesu.
Ameni.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.