TB JOSHUA AELEZA KILICHOSABABISHA JENGO LAKE KUANGUKA



Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria, jumapili iliyopita aliweka bayana kilichosababisha jengo la hosteli ya kanisa lake kuanguka na kuua watu zaidi ya 100 akiweka wazi kwamba waliotenda jambo hilo wanalenga kummaliza yeye na si watu wengine. Tukio la kuanguka kwa hosteli hiyo inadaiwa kusababishwa na ndege kubwa iliyokuwa ikipita usawa wa chini kabisa wa jengo hilo zaidi ya mara mbili kabla ya jengo hilo kuanguka na ndege hiyo haikurudi tena.

TB Joshua ameeleza kupokea simu mara mbili kabla ya tukio hilo watu hao wakitaka kujua alipo ili kutenda jambo lao na yeye kujibu kuwa yupo mlimani kuomba, ambapo ndege hiyo ikawa inapita maeneo ambayo mtume huyo alienda kuomba lakini kumbe wakati huo alishamaliza na kurudi kanisani na alipopigiwa tena akajibu yupo kanisani ndipo ndege hiyo ikahamia juu ya jengo hilo na kutokea yaliyotokea huku mtume huyo akinusurika.

Kutokana na maelezo ya TB Joshua inawezekana tukio hilo limetendwa na wanajeshi wa kundi la kiislamu la Boko Haram ambao wamekuwa wakitafuta namna ya kumuangamiza hasa baada ya baadhi ya wanajeshi wake waliotumwa na kundi hilo ili kummaliza wakajikuta wanafichua siri zote na kuachana na mpango wa kumuua mtume huyo. Aidha katika video iliyopo chini ni tukio zima la mtume huyo akizungumzia kilichojiri katika tukio hilo ambalo limetikisa Afrika kutokana na umaarufu wa mtume huyo.




Baada ya tulio hilo ambalo lilishuhudia raia wa wengi wa Afrika ya kusini waliofika kanisani hapo kwa maombi kufariki dunia, serikali ya Cameroon kupitia waziri wake wa mambo ya nje alitoa tamko la serikali la kuwakataza raia wa nchi hiyo kwenda kwa mtume huyo wakidai anatumikishwa na shetani na kwa yeyote atakaye kaidi tamko hilo basi lolote litakalomkuta serikali ya nchi hiyo haitowajibika naye(Kama hukusoma bonyeza Hapa). TB Joshua ni mmoja kati ya wahubiri wanaopata upinzani mkali juu ya anayewawezesha kufanya miujiza mikubwa ya uponyaji, lakini bado ameendelea kusimama na wito wake katika kuhubiri injili ya Kristo.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.