UJUMBE: KUTIWA NGUVU IMANI YAKO KWA KUTOANGALIA TATIZO BALI KUMWANGALIA YESU


Ujumbe kutoka kwa mtumishi King Sam

Unaweza kuwa kwenye tatizo lakini usiangalie hilo tatizo bali mwangalie YESU amesemaje katika hilo tatizo.

Tutaangalia watu ambao waliangalia Mungu alichosema wakapokea sehemu Yao Kama wewe unavyo weza kupokea sehemu yako Kama tu utaangalia Yesu pale msalabani alikuja kufanya nini kwa ajili yako,ukiangalia tatizo linakumeza,lakini katika Jina la Yesu upate Neema ya kuweza kumwalia Yesu na kumuamini ili uhesabiwe haki kwa kile ulichokiangalia na kukiamini kupitia Yesu.

Ibrahimu alihesabiwa haki kwa kuangalia ahadi za Mungu juu yake na kuamini kwamba Mungu anaweza kufanya kile alichoahidi,

Warumi 4:19-22
Biblia inasema Ibrahimu alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa na akiwa amekwisha kupata umri Wa miaka Mia,na hali ya kufa ya tumbo la Sarah,hakujali hivyo vitu Bali aliangalia ahadi ya Mungu kwa hiyo akatiwa nguvu katika imani kwa kuona Mungu alichosema,

Watu wengi tumekuwa tunashindwa kwa sababu hatuangalii ahadi ya Mungu Kwetu bali tunaishia kufikiria tatizo lililo tusonga mwisho tatizo linatumeza,katika Jina la Yesu kristo naomba upate Uwezo Wa kuangalia kile Yesu alichosema ili upokee kiwe chako katika Jina la Yesu,


Hesabu 21:8-9 Wana Wa Israel waliumwa na nyoka Mungu akamwambia Musa ajifanyie nyoka Wa Shaba na kuiweka juu na kila aliye umwa aitazamapo ataishi.

Ndugu yangu unaweza ukawa umeumwa na tatizo lolote labda ni Ugonjwa au ndoa au biashara au kazi au mke hana mtoto au matatizo mengine,Yesu anajibu lako pale msalabani inua macho yako umtazame, usitazame ilo tatizo Wala huyo nyoka aliye kuuma Bali mtazame Yesu,wale wana Wa Israel waliotazama nyoka Chini walikufa lakini wale waliyo tazama nyoka Wa Shaba juu waliishi,unaweza kuishi tu pale utakapomtazama Yesu,usitazame Dakitari amesema nini Wala wanadamu wanasema nini Bali tazama Yesu anajibu lako,tatizo lipo lakini usiishie kulifikiri Bali nyanyua macho yako utazame ahadi ya Mungu,Ibrahimu hakuishia kufikiria alivyo kuwa Wala mke wake alivyokua Bali aliangalia ahadi ya Mungu na kuamini Mungu anaweza akahesabiwa haki kwa hivyo,hata wewe unaweza kuhesabiwa haki ya kuwa mzima kuwa mwenye watoto kuwa mwenye biashara kuwa mwenye mafanikio kwa njia tu ya kutazama Mungu amesemaje na ukaamini Mungu anaweza kufanya,usitazame madakitari wamesemaje juu yako Wala usitazame dunia inasemaje kwa uchumi ndugu zangu tumtazame Mungu na ahadi zake juu yetu na kumuamini anaweza kufanya alichoahidi katika Jina la Yesu sema amen.

(Yesu anasema mimi nalikuja ili muwe na Uzima kisha muwe nao tele)
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.