WANAJESHI WAKIRI HAKUNA KAMA JEHOVAH

Sehemu ya umati wa wanajeshi hao ukiendelea na sifa. ©The Church Guide screengrab
Huku mtaani, inafahamika kwamba wanajeshi hawana mzaha, ni wakakamavu muda wote, na wako na sura ya kazi popote pale utakapowakuta, (hata kama wanatembea tu). Ili mradi ukiona uniform ipo basi pengine unajisemea, "ngoja nikae mbali".

Hakuna kama Jehova... ©The Church Guide screengrab
Kwa wale waliosoma shule za jeshi pia wanajua, ya kwamba amri ndo zinafanya kazi, unatekeleza jambo kwanza kisha maelezo baadae. Maana hata kama hujapitia shule hizo, yawezekana umeona kwenye maadhimisho ya mbalimbali ya taifa hili la Tanzania, pale ambapo matofali yanavunjwa kwa wepesi kama mihogo.

Lakini kwa video ambayo GK imekutana nayo kwenye mtandao inahamasisha kwa kweli, maana wanajeshi ndani ya sare zao wakilitukuza jina la Mungu. Days of Elijah ndio wimbo ambao wanajeshi hawa wanarejea kumtukuza Mungu.


"There's no god like Jehovah, theres no god like Jehovah… Behold he comes…" ni sehemu ya kipande cha wimbo huo maarufu ambao umeshaimbwa na waimbaji mbalimbali ikiwemo pia kutafsiriwa kwa lugha mbalimbali ikiwemo Kiswahili, ukiimbwa, "Hakuna kama Jehovah, hakuna kama Jehovah..."

Kwa mujibu wa mwanamama, Merrie Pardee Baldwin ambaye aliweka video hii hewani kwa mara ya kwanza anaeleza kwamba anatamani taifa lao liombee vikosi hivyo ambavyo viko kwenye shughuli ya kulinda amani ya taifa na dunia kwa ujumla, huku hofu kubwa ikiwa ni kuhusu kikundi cha kigaidi cha ISIS ambacho kinatatiza.

Faith Warriors, ama Mashujaa wa Imani kwa lugha ya Kiswahili, ndio ratiba amayo iliwafanya wanajeshi hao takribani 500 wakusanyike na kuimba kwa umoja wao, huku pia muda mwingine wakiweka vionjo vya kijeshi-jeshi na kupunga mikono hewani wakisema "Ooh Rah", kila baada ya kipande cha 'lift your voice'.

Video hiyo si tu kwamba inapendeza kwa kinachoendelea, bali pia imeibua hisia kwa watu kadhaa, wengine wakijieleza kwamba walishindwa kuzuia machozi yao pale walipoona wanajeshi hao wanalisifu jina la Yesu, licha ya kwamba huenda miongoni mwao wengine walikuwa wanafatisha tu.

Basi wacha Neno la Mungu liendelee kutimia, maana kila mtu atakubali tu, iwe kimoyomoyo ama waziwazi, itabaki hivyo, kwamba hakuna Mungu kama Jehova!

Christian Post imeandika.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.