WORSHIP IN YOUR PRESENCE NDANI YA CCC UPANGA OKTOBA 5

Kati ya mambo ambayo unatakiwa kujipanga kwayo ni tamasha la kusifu na kuabudu, lililopewa jina la Worship in your Presence, litakalofanyika tarehe 5 Oktoba kwenye ukumbi wa kanisa la CCC Upanga, ambapo jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake litashuhudia kundi la waimbaji mahiri wakimsifu na kumuabudu Mungu siku hiyo, ambapo waimbaji kama Glorious Worship Team, Emmanuel Mbasha na Flora Mbasha watakuwepo, ukiachilia mbali ambao wametajwa na kuwekwa picha zao kwenye chapisho la tamasha na huku pia wengine wakiendelea kuweka ratiba zao sawia ili wasikose tukio hili muhimu, GK imefahamishwa.

Tofauti na matamasha mengine ya kawaida, kuna vitu ambavyo kwa hakika vimekaa sawa kwa mujibu wa waandaaji wa tamasha hilo, ambalo linategemewa kuvunja rekodi kadhaa, ikiwemo

1. Kutoa tuzo kwenye tamasha; ambapo muimbaji nguli wa nyimbo za injili, John Lisu anatarajiwa kupewa tuzo ya heshimakwa mchango wake kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini.

2. Kutakuwa na red carpet, ambapo watu wanaingia na kupiga picha pamoja na waimbaji mashuhuri kabla na baada ya tamasha.

3. Usafiri Dar es Salaam, (UDA) watasafirisha watu kutoka maeneo mbalimbali ya jiji na kuwafikisha, ambapo magari hayo yatakuwa na machapisho kuhusu tamasha hilo. Na kisha baada ya hapo mabasi yatakuwa tayari kurejesha watu makwao kuanzia saa tatu kamili usiku, ambapo yatakuwa yameanza kufika maeneo ya kanisa.

Pamoja na waimbaji wengi kuonyesha nia ya kushiriki tamasha hilo, mwenyekiti wa baraza la makanisa ya Kipentekoste nchini Tanzania (CPCT), kwa mkoa wa Dar es Salaam, Askofu Bruno Mwakibolwa atakuwepo kutoa Neno la utangulizi kabla ili kushusha uwepo wa Mungu mahala hapo kwenye tukio zima.


Endelea kufuatilia GK, nasi tutakufahamisha taarifa za maendeleo ya tukio hili kama ambavyo litakuwa likitufikia - na kwa kadri ya waimbaji zaidi watakavyokuwa wakithibitisha ushiriki wao kwenye tukio hili la kihistoria, kabla ya kluhamia jiji la Arusha mnamo Novemba.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.