ANGALIA WAIMBAJI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA JAPAN WAKIIMBA MKOANI TANGA

Angalia baadhi ya picha za kundi la kusifu na kuabudu kutoka kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Japan ambao wapo mkoani Tanga katika mkutano wa injili ulioandaliwa na tawi la kanisa hilo mkoani Tanga wakiongozana na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo duniani Josephat Gwajima ambaye siku ya jumanne alifundisha somo lenye kichwa kisemacho 'Madhabahu ya kushindwa' ambalo unaweza kulisoma chini ya picha zifuatazo.


NA MCH. KIONGOZI: JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: MADHABAHU YA KUSHINDWA

Utangulizi
Madhabahu - sehemu aliyoiandaa mtu kwa ajili ya kutolea kafara zamani watu waliotolewa kafara ili waweza kushinda vita
2Wafalme 3:20-27......[ mstali 20:27]
Mtu anapo kushinda ujue ametowa kafara kwenye Madhabahu
Matendo 7:43.......[mstali 43] '' Nanyi mlichukua hema ya Moleki Na nyota za Mungu wenu Refani, Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu: Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.
Kitu gani kinachofanya kazi kwenye Madhabahu ni Damu.

Mtu anapotaka kuku haribia maisha yako huchinja mnyama ili damu imwagike
Walawi 17:10-14......[mstali 10-14] '' Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu ya aina yo yote, nitakuja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake. 11. Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya Madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajiliya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisha kwa sababu ya nafsi.12. kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu, wala mgeni aketiye kati yenu asile damu. 13. Mtu ye yote aliye wa wana wa Israeli, au wa hao wageni wakaao kati yenu, ambaye huliwa, katika kuwinda kwake; atamwaga damu yake, na kuifunika mchanga. 14. kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake;atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali
Mwanzo 9:4.........[mstali 4] '' Bali nyama pamoja na uhai, yaani.damu yake, msile .
Damu inapa nguvu madhabahu kwauhaii sababu damu ni uhai
Damu ina sauti
damu inaweza kusikika
Mwanzo 4:10.......[mstali 10] ''Akasema umefanya nini ? sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katiks ardhi.
Madhabahu inauwezo wa kuharibu maisha ya mtu
Damu ya Yeu inauwezo wa kuzungumza mema.
Ili uibomoe Madhabahuya kushindwa ni lazima uibomoe kwa jina la Yesu . AMEN
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.