BREAKING NEWS: RAIS WA ZAMBIA AFARIKI DUNIA

Hayati Michael Sata ©Lusaka Times
Habari za kusikitisha ambazo zimethibitishwa na Katibu wa baraza la mawaziri, Dkt. Roland Msiska, zinaeleza kwamba Rais wa Zambia, Michael Sata, amefariki dunia akiwa kwenye matibabu kwenye hospitali ya King Edward VII, jijini London, Uingereza alikoenda tarehe 20 Oktoba kwa ajili ya matibabu.

Michael Sata ambaye amekuwa madarakani mwezi Septemba 2011, ameripotiwa kufariki dunia Oktoba 28 2014, ambapo hivi karibuni kulikuwa na uvumi nchini kwake ya kwamba yuko hoi kwa magonjwa, kiasi cha kushindwa kuonekana hadharani tangu aliporejea kutoka kwenye mkutano mkuu wa nchi wanachama za Umoja wa Mataifa (UN), nchini Marekani.

Michael Sata amefariki akiwa na umri wa miaka 77, na kuacha mjane, Christine Kaseba na watoto zaidi ya 15. Makamu wa Rais Guy Scott anakaimu nafasi kwa sasa.

Makamu wa Rais, ambaye kwa sasa atashikilia kiti cha urais, Guy Scott ©Zambia Daily Nation

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.