CHAGUO LA GK JUMAPILI YA LEO UNGANA NA WAIMBAJI HAWA


Chaguo la GK jumapili ya leo tupo na kwaya inayofanya vizuri sana kwenye medani ya muziki wa injili nchini nao si wengine bali wana wa AIC Shinyanga Choir ambao wimbo wa Ng'ang'ania Baraka za Bwana uliwatambulisha vyema kwakila mpenzi wa muziki wa injili nchini.

Siku ya leo nimekuchagulia moja kati ya wimbo wao unaowabariki watu wengi sana uitwao 'Nalilia Uzima' ambao unapatikana katika album yao ya 'Mbeleko'. Wimbo huu una maneno mazuri sana ambayo hutusogeza mbele za Mungu wetu kwa ushindi mkuu bila kuogopa jambo lolote. Kwasasa kwaya hii inajiandaa kutoa video mpya, wakumbuke kwenye maombi yako

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.