CHAGUO LA GK: PITSON NA LINGALA YA YESU

Twatumai u mzima mdau wa GK, karibu kwenye Chaguo letu wiki hii liko kwa Pitson, muimbaji kutoka nchini Kenya, na hapa akielezea kuhusu lingala ya Yesu. Ukisikiliza wimbo huu utatambua ya kwamba Pitson anakumbusha kwamba haijalishi ni namna gani tunamsifu Mungu, na wala haihitaji matayarisho yenye gharama mno - ila kinachohitajika ni kujitoa kwake na kumtukuza kwa namna yoyote uwezavyo.
Wakati unasikiliza na kutafakari maneno ya Pitson, chukua hatua na ukajiachie kwa Bwana Yesu kwa namna uwezavyo na hatimaye utukufu umrudie yeye anayestahili sifa zote. Tunaamini batoto wa GK bataipenda... Jumapili njema.


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.