HILLSONG YAVUNJA REKODI MAREKANI, KUNDI LAKE PIA LAONDOKA NA TUZO TANO

Moja ya ukumbi uliojaa watu wakifuatilia kongamano la Hillsong.
Kanisa linaloendelea kukua duniani la Hillsong lenye makao makuu yake nchini Australia limejivunjia rekodi yake nchini Marekani baada ya kuuza tiketi zote kabla ya kuanza kwa kongamano kubwa linaloanza kesho katika ukumbi mkubwa uliopo Madison Square jijini New York.

Kongamano hilo kubwa ambalo linafanyika mara ya pili nchini Marekani limepewa jina la 'No Other Name' jina ambalo pia limebeba album mpya ya moja ya makundi ya kanisa hilo lijulikanalo kama 'Hillsong Worship'. Hillsong walifanya kongamano la kwanza mwaka jana katika ukumbi wa Radio Music City huku ikiripotiwa watu zaidi ya 7000 waume kwa wake walihudhuria.

Ambapo katika kuwapa nafasi watu wengi zaidi, kanisa hilo tawi la New York limeamua kuandikisha majina ya watu wanaotaka kuhudhuria kongamano hilo ili wapatiwe tiketi endapo kutatokea watu walionunua tiketi wanataka kuziuza au kugawa kwa watu wasionazo endapo watapatwa na dharula.


Aidha wakati hayo yakiendelea, kundi la Hillsong United liliondoka na tuzo 5 kati ya 10 ilizokuwa ikiwania baada ya kupendekezwa kuwania tuzo za Dove awards ambazo zilifanyika kwa mara ya 45 tangu kuanziashwa kwake. Tuzo hizo ambazo zimefanyika huko Nashville Tennessee, ambapo kundi hilo liliondoka na tuzo ya kundi bora la mwaka, kundi bora ka Kikristo kwa upande wa uimbaji, huku wimbo wao wa 'Oceans' ukibeba tuzo tatu moja ikiwa wimbo bora wa mwaka, wimbo bora wa kuabudu wa mwaka na wimbo bora wa aina ya pop na kurekodiwa vyema.

Kundi hilo limeshukuru kwa kupata tuzo hizo kupitia mchungaji JD aliyesema anamshukuru Mungu kwa heshima kuwa miongoni mwa maelfu ya watu wanaojitoa kupeleka injili kupitia kanisa hilo kwa zaidi ya miaka 30 sasa. kwakuwa kujitoa kwao kunalifanya kanisa lao kuwa imara zaidi.Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.