IMANI YA KIMUNGU - MCHUNGAJI JOSEH JONES


Kama wewe ni raia wa Tanzania unahitaji upate fedha kupanda daladala na kuishi lakini kama wewe ni raia wa mbinguni hauhitaji fedha kwenda mbinguni na fedha ya ufalme wa Mungu ni Imani. “Biblia ina sema mwenye haki wangu atatembea kwa imani” na wala hatuwezi kuingia katika ufalme wa Mungu bila imani.

Waefeso2. 8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;

Waebrania11: 1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. akini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Kama unataka kumpendeza Mungu lazima uishi kwa imani na ndani kuna uponyaji, wokovu, amani, nguvu na pasipo kutumia imani huwezi kupokea Baraka hizo. Tunahitaji kuwa na uvumilivi
Warumi1: 17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.

Imani inakuja kwa kusikia neno la Mungu na hiyo ndiyo njia pekee unayoweza kupokea imani kwa kusoma neeno la Mungu, kutafakari na kulitenda neno la Mungu na imani. Nenda kwenye ATM ya Mungu (Biblia) na uchukue imani. Neno la Mungu ni mbegu na Yesu alisema mfano wa mpanzi aliyeenda kupanda mbegu

Marko4: 13 Akawaambia, Hamjui mfano huu? Basi mifano yote mtaitambuaje? Mpanzi huyo hulipanda neno. Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao. Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye miamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, mara hulipokea kwa furaha; ila hawana mizizi ndani yao, bali hudumu muda mchache; kisha ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara hujikwaa. Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikiao lile neno, na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai. Na hawa ndio waliopandwa penye udongo ulio mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, mmoja thelathini, mmoja sitini, na mmoja mia. Akawaambia, Mwaonaje? Taa huja ili kuwekwa chini ya pishi, au mvunguni? Si kuwekwa juu ya kiango? Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila makusudi lije likadhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila makusudi lije likatokea wazi. Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.

Neno la Mungu ni mbegu ambayo siku zote hutenda kazi. Tunalipanda neno la Bwana ndani ya mioyo Yetu na mbegu ya Mungu itakuwa ndani ya mioyo yetu tukiipanda na kama tukipanda viazi je vitakuwa mahidi? Jibu ni Hapana! bali vitakuwa viazi, na tukitaka imani lazima tupande neno la Mungu ndani ya mioyo yetu.

Ndani ya mioyo yetu tukipanda neno la Mungu mara kwa mara baadaye mti wa imani utaanza kukua. Lazima tuwe wavumilivu na tuusubiri ule mti wa imani kwenye mioyo yetu uanze kukua. Kwa imani na uvumilivu tutadiriki Baraka za Mungu.

Yakobo1: 21 Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.

Tunataka kukombolewa tulipokee neno la Bwana na lianze kukua, kazi yetu ni kulisikia neno la Mungu kila siku na ni kazi ya Mungu kulifanya neno lake likuwe ndani yetu hivyo kazi yetu ni kulifanya.

Warumi10: 8 Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Imani ni kuamini kwa mioyo yetu na kuongea kwa midomo yetu na wakati watu wanakuambia kuhusu kuokoka wanapanda mbegu ndani ya moyo wako hivyo kwa kuamini ndani ya mioyo yetu na kwa kukiri kwa midomo yetu linakuwa sawasawa na tunavyoamini. Kama unataka furaha ni hivyohivyo. Tunatakiwa tuwe wajawazito wa imani na kuzaa imani kwa vinywa vyetu kwamba nimebarikiwa kwa jina la Yesu, nimefanikiwa kwa jina la Yesu, nimepona kwa jina la Yesu.

Yesu alizungumza katika mji mmoja unaitwa Bethania na kila siku alitembea kwenda Israeli kuhubiri injili na kufundisha na jioni anarudi bethania kulala na siku moja aliuona mti na Biblia inasema haukuwa msimu wa mti kuwa na matunda na Yesu hakuona tunda kwenye mti ule na akaulaani kuanzia siku ile usizae tena na akaenda zake na kesho yake asubuhi akapita na wanafunzi wake wakamwambia ule mti umekauka na Yesu akasema Ukiamini na kusema kwa imani inakuwa vile utakacho kisema.

Mtu anaweza kujisikia kama anaimani lakini ni mtupu unaweza kusema kuhusu kukombolewa lakini kama hupandi neno ndani ya moyo wako huwezi kuwa mjamzito wa imani na kuzaa na Biblia inasema imani hiyo ni imani iliyo kufa. Biblia inasema usimsahau Mungu akuponyaye magonjwa yako yote na kukusamehe makosa yako yote, unatakiwa useme kwa kupigwa kwa Yesu mimi nimeponywa. Biblia inasema ukiwa na imani ndani yako chochote utakachokisema utakipata sawa sawa na imani yako kama usemavyo.

Inawezekana unasema mimi ninaamini lakini siwezi kukisema ninachokiamini sababu kama kisipotokea nitachekwa na watu wengi kwenye imani wanasema wanaamini lakini kusema ni vigumu. Unalisikia neno unalipanda ndani ya moyo wako alafu unalisema. Kama unataka ulinzi unasema mabaya hayatanipata mimi wala tauni haitakaribia hemani mwangu, hakuna uchawi juu ya Yakobo wala uganga juu ya Israeli unalisoma mara nyingi na unaanza kulitamka. Kwenye ufalme wa Mungu thamani yake ni Imani na kwenye kupanda mbegu ya imani ndani yetu kuna muda wa kusubiri ikue kama unavyo panda mbegu ya mmea na ikachukua muda fulani kukua. Mungu aliumba kwa kusema na unatakiwa uwe mtu wa kusema sema na itakuwa vile vile uaminivyo kwa jina la Yesu.

Imeandikwa mabaya hayatanipata mimi wala tauni haitasogelea hemani mwangu kwa jina la Yesu sita kufa bali nitaishi imeandikwa hakuna uganga juu ya ya Israeli wala uchawi juu ya Yakobo "tamka maombi ya imani huku ukiamini na itakuwa vile vile unavyosema kwa jina la Yesu kristo

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.