ISIS WACHINJA WATU KUMI NA KUMSHUKURU 'MUNGU' WAO

Baadhi ya wanakikundi wa kundi la kigaidi la ISIS ©Vice News
Kama kuna jambo ambalo linaendelea kuumiza vichwa vya watu, basi ni uwepo wa kundi la kigaidi linalojiita ISIS - Islamic State of Iraq and Syria, ambao wanaendelea na mauaji yao, kwa sasa wakichinja watu kumi, watatu miongoni mwao wakiwa wanawake magharibi mwa mji wa Kobani, mji wa Kikurdi nchini Syria.

Mauaji yao ambayo hufanyika hadharani na mara kadhaa kurekodiwa na kuwekwa mitandaoni, wana kauli mbiu ya kwamba, ukileta vurugu unamalizwa, na hata usipoleta vurugu utamalizwa pia kwani matendo hayo hayo hayavumiliki.

Kwa mujibu wa mwangalizi wa haki za binadamu nchini Syria, Rami Abdulrahman, amesema kwamba hajajua sababu ya tukio hilo, lakini anaamini ni kwa ajili ya kutishia ulimwengu.

Haijajulikana kwa sasa kusudi la kuchinja watu hao ilikuwa ni nini, ila tukio hilo limeelekezwa kuwa ni hasira ya kushambuliwa kwa anga na taifa la marekani na washirika wake ikiwemo Ufaransa na Uingereza.
Bendera ya ISIS (nyeusi) ikipepea sanjari na bendera ya Kikurdi ©Charisma News
Aidha pamoja na mashambulizi hayo, ISIS wamekuwa wakikejeli mashambulizi hayo na kusema kuwa vita ya kweli ni ya ardhini na si angani kama wafanyavyo 'wabaya' wao, na pia kwamba wao wanamshukuru mungu kwa kuwa mashambulizi yao hayana madhara yoyote - ni sawa na kupoteza muda.

Charisma News | Christian Headlines
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.