JINSI YA KUTAMBUA KAMA UNA LAANA YA KUTOOLEWABWANA YESU asifiwe!
Karibu ujifunze kitu hapa ambacho kitakusaidia kuweza kufuta laana za kukuzuia kuolewa/kuoa.
Laana ni kitu kinachokushika ili usifanye jambo Fulani jema.
Laana ni mfano wa ndege aliyefungwa kamba ndefu mguuni kwenye mti , hutoka na kupaa karibu tu na kurudi kwenye mti , hawezi kwenda zaidi. Na mtu mwenye laana ya kutokuolewa/kuoa hupata mateso makubwa sana .

Ni kama yuko huru lakini kuchumbiwa/kuchumbia ni mtihani, na hata akichumbiwa/Kuchumbia kabla ya kuolewa/Kuoa uchumba unavunjika, au akiolewa tu anaachika au mme/Mke anakufa kifo cha ghafla cha mapema. Kuna haja ya kujifungua kutoka kwenye laana zote ikiwemo laana ya kutokuolewa/Kuoa. laana hii katoa nani? Yawezekana adui za wazazi wako, yawezekana mababu katika ukoo, yawezekana wachawi, yawezekana maadui wa ukoo wako , yawezekana maadui wa familia yako, yawezekana majini mahaba ya ndotoni, yawezekana waganga wa kienyeji, yawezekana ni mizimu au shetani mwenyewe na yawezekana mtu yeyote mwenye nia mbaya na ukoo wenu au nia mbaya na familia yenu au nia mbaya na uzao wa tumbo la mama yako na wewe ukiwamo ndani yake.
Unaweza kuepuka laana au mikosi ambayo ni kisababisho cha mateso wakati wa kuoa/kuolewa kama mmoja kati ya wanaooana yuko kwenye mkondo wa laana.

NJIA KUMI(10) ZA KUTAMBUA KAMA UNA LAANA YA KUTOKUOLEWA.
1. Ukiwa na ndugu wa kike zaidi ya wawili wakubwa, wenye miaka 30 na zaidi, ambao hawajawahi kuchumbiwa kabisa.
2. Kila unapokaribia kuolewa katika zaidi ya matukio mawili, mara zote huishia kukatishwa tamaa na uchumba wako kuvunjika bila sababu za kueleweka.
3. Endapo kuna hali inayoashiria kifo cha ndoa, na ambayo huharibu ndoa kabisa.
4. Hata kama ni mwanamke mzuri na mwenye mwenendo mzuri na maisha ya maadili mema, utaona kabisa hakuna kijana anayevutiwa na wewe ili kukuchumbia muoane. Hata kwa wale wenye nia ya kukuchumbia hujikuta wakitoweka tu bila sababu.
5. Endapo Baba au Mama yako , au mtu mwingine akitoa laana ya maneno kuhusu wewe kuolewa.
6. Ikiwa msichana yeyote katika familia yako kaolewa katika mazingira magumu au wale ambao hufa vifo visivyoelekea tena muda mfupi tu baada ya kuolewa.
7. Endapo utasikia sauti ikisisitiza kukuambia kuwa ‘’Kamwe hutaolewa’’ au ‘’Kamwe hutapata mafanikio kwenye maisha yako.’’
8. Ikiwa una pepo mume au watoto wa kipepo. Kwa mfano katika ndoto unazoota utaona mwanamume akija na kufanya mapenzi na wewe, au kujiona una ujauzito na hatimaye kuzaa watoto katika ulimwengu wa roho yaani katika ndoto. Wakati mwingine , mtu huyo anaweza hata akajidhuhirisha katika ulimwengu wa Mwili.
9. Kama hupati kabisa siku zako za mwezi(Hedhi).
10. Kama wewe huota ndoto zenye kuogopesha hususani kuota unacheza na nyoka au viumbe wenye kutambaa.

JINSI YA KUFUTA LAANA .

Kama ukigundua kuna laana katika maisha yako.
1. Hatua inayofuata ni wewe kwenda kufanyiwa maombezi.
2. Kukutana na mtumishi aliyeokoka ambaye atakuongoza kwenye maombi yanayohusiana na ukombozi na tatizo lako litaisha kwa jina la YESU KRISTO.
3. Marko 16:15 YESU KRISTO anasema ‘’Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio, Kwa jina langu watatoa pepo’’
4. BWANA YESU anaendelea kusema ili kuondoa ushetani huu katika maisha yako anasema katika Luka 10:19 ‘’ Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. ‘’
5. Okoka na baada ya hapo tumia hata siku 3 za kufunga na kuomba maombi ya nguvu, huku ukijiambatanisha na MUNGU huku ukifukuza kila aina ya mapepo na kuharibu mamlaka yao inayofanya kazi katika maisha yako, haribu kwa jina la YESU KRISTO.
6. Kuhusu majini mahaba yakatae na kwa jina la YESU KRISTO. Na bila huruma muombe ROHO MTAKATIFU ashushe moto na kuharibu masalia ya majini mahaba.
7. Epuka mawazo ya ngono na badala yake akili yako ijazwe Neno la MUNGU pamoja na nyimbo za kuabudu.
- Kila siku funika kitanda chako kwa Damu ya YESU KRISTO kwa njia ya maombi.
8. Dumisha utakatifu na uwe mwana maombi siku zote, omba katika ROHO MTAKATIFU na tumia mamlaka ya YESU KRISTO kujiweka huru siku zote.


Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

mabula1986@gmail.com

MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.