KATIBA INAYOPENDEKEZWA HII HAPA

Rais Kikwete akipokea Katiba inayopendekezwa kutoka kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta.
Tarehe 8 Oktoba ndani ya jiji la Dodoma, ndipo ambapo Katiba inayopendekezwa ilikabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete, na Rais wa Zanzibar, Ali Mohammed Shein.

Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali na kisha kufuatiwa na tafrija fupi ikulu ya Chamwino, ilipokelewa kwa hisia tofauti na wananchi, baadhi wakipongeza hatua ya taifa la Tanzania kuandika historia mpya, huku baadhi wakisitika namna mchakato ulivyopelekwa bila maridhiano kiaso cha kupoteza mabilioni ya fedha za walipakodi.

GK inakuwekea Katiba inayopendekezwa ili upate kuisoma na kuweza kujua nini kinaendelea kwa sasa nchini. 


Pamoja na hayo pia tunakuwekea Rasimu ya Pili iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa inaongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Jaji Jospeh Warioba akimkabidhi Rais Kikwete Rasimu ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Disemba 2013 jijini Dar es Salaam.Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.