KUKUA NI MCHAKATO, SI MUUJIZA

Uko hatua gani? © Never Growing Old Blog
Na Faraja Naftal Mndeme

Katika namna ambavyo mfumo wa kuishi umewekwa na uhalisia wa mambo ulivyo katika sayari yetu iitwayo Dunia, kukua ni mchakato na sio muujiza. Kitu chochote ili kikue kufikia utimilifu lazima kinapitia mchakato fulani kabla ya kufikia ukamilifu wowote. Hakuna kitu ambacho kinaweza kukua ghafla bila kupitia mchakato wa aina yoyote, iwe ni kiroho au kimwili. Binadamu ili kufikia hatua ya kukua na kufikia na ukamilifu wake lazima kuna hatua na mchakato fulani amepitia. Lazima mtoto azaliwe, akue na kufikia ujana. Uzee ndio unakuwa tamati na kifo huchukua mkondo wake.

Katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukikumbana na changamoto na vitu mbalimbali ambavyo tunashindwa kuelewa kanuni za msingi za kuendesha vitu. Katika kila unachofanya lazima kwanza kinaanza na kuzaliwa, hatua ya katikati ndipo utimilifu wa juu wa kitu hufikia. Unapomuona mtu mzima leo (Mzee) lazima alipitia hatua zote tatu muhimu.


1. Kuzaliwa
Kuzaliwa ni moja ya hatua muhimu ya maisha na uhai wa kitu chochote,katika hatua hii unaweza ukawa umependa kitu kizaliwe au kisizaliwe lakini mwisho wa siku wote tunajikuta kwenye uwanja wa Mapambano. Je unaendelea kulaumu kwa nini kitu fulani kilizaliwa? Hapana, yaani hata kama ukilaumu ndio tayari kimeshaonekana kwenye ulimwengu wako.

Mfano kuna watoto walizaliwa kwa uzazi wa mpango na wengine ghafla bin vuu wakajitokeza kwenye hii sayari. Aliyezaliwa kwa uzazi wa mpango na wa Ghafla bin vuu mwisho wa siku wote wako kwenye sayari hii itwayo Dunia. Kulaumu kwako hakukufanyi urudi tumboni kwa mama bali ndio umeshafika sasa.

Yaani Samaki aliyevuliwa kwa baruti na wengine kwa njia sahihi lakini mwisho wa yote wamevuliwa na wameshatolewa baharini.

Hapa ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu ya kawaida unaweza ukapanga kufanya kitu fulani kwenye maisha au Usipange lakini mwisho wa siku ndio umeshajikuta humo. Je Unafanyaje? Kulaumu hakutasaidia kutatua hilo tatizo au hicho kitu ambacho umekutana nacho.

Kitu kinapozaliwa kinaweza kisiwe na mwelekeo sahihi lakini wewe mlezi wa kitu ndio una uwezo wa kufanya kitu kiwe sahihi,ndio Maana Wahenga husema Mtoto uleavyo ndivyo akuavyo. usitegemee Utamlea mtoto katika hali ya uvivu na Uzembe alafu akikua awe Mchapa Kazi...
Unapotaka kuanza Biashara lazima Izaliwe kwanza,Unapotaka Kuanza kazi lazima iwe na mwanzo wake...Hakuna kitu kina kua tu...Kumbuka Hata Mbuyu ulianza kama Mchicha Ila Sijui...Kiroboto alianza kama nini....mwisho wa Siku Kukua ni Mchakato na Sio Muujiza...


2. Kukua
Siku hizi kwenye jamii kumekuwana matatizo mengi sana ambayo watu wengi tumeshindwa kupata majibu kwa sababu hatujui mchakato wa vitu hivyo vimeaanzi wapi,Mfano Wakati unakuwa nyumbani kwenu unakuta Style ya Maisha ni Matusi na Ngumi kuanzia kwa Baba na Mama Mpaka Kaka/Dada zako.Je Unahisi hapa itakuwaje?Je unapomwona Mtu ni Mlevi unahisi alinza ghafla tu..Hapana Kukua kwenye jambo lolote ni Mchakato na sio Muujiza hata Ukisoma kwenye Vitabu vya Dini Dhambi ili iwe dhambi Kuna mchakato imepitia mpaka kufikia Tamati

Kufikia hatua ya kukua kwenye kila jambo inategemea msingi uliojengwa tangu mwanzo wakati jambo linaanza..Unaapomwona mfanyabiashara mkubwa leo amefanikiwa hakuanza kama uyoga bali kuna mchakato alioupiti kugia Hapo.Mara nyingi tunasahau kwamba hakuna kitu ambacho kinaibuka tu kwenye maisha Yetu ya kila Siku..tangu Mwanzo ukijenga tabia ya kusoma vitabu na kutafuta maarifa na kubuni vitu na ukaendelezwa ndivyo utakavyokua.

Usimshangae mtu alivyo Leo Maana Hukuona Jana Yake,Tabia na Maisha ya Mtu ilivyo leo Inatagemea kwenye hatua za mwanzo alianzaje?

Mara nyingi nimekuwa nikipishana na watu sana kwenye kuwahukumu watu kwenye maisha yao kwa sababu sisi tunaona matokeo lakini hatujui huyu mtu alianzaje...Imekupasa kulaaumu msingi wake ulivyojengwa na sio hii hatua ya Katikati ya Kukua.


3. Ukomavu
Hatua iliyopita ni moja kati ya hatua muhimu ambazo zinaweza zikatoa Majibu ya maswali mengi kufikia kuelekea hatua hii ya Ukomavu(Maturity).

Kutokana na mfumo wa Malezi yetu Watanzani kama si waafrika tulio wengi tunakuja kugundua vitu vingi si sahihi kwenye hatua ya Kukua wakati msingi ulishajengwa vibaya.Mfano wa Ghorofa Ikishajengwa vibaya toka chini kwenye Msingi ndivyo itakavyoendelea Mbele kwenye Ujenzi.Iwapo Fundi hakushtuka basi ujenzi huo utaendelea mpaka mwisho wa safari na Mwisho wa Siku tunashuhudia Ghorofa zinaanguka na kuua watu.

Pamoja na maisha yetu ya kila siku kujengwa Hivyo mpaka tikufikia ujana ndio tunagundua kwamba hiki hakikuwa sahihi Je unafanyaje?Je unaendele kuishi kwenye Ubaya?Je Unavunja Msingi huo Uanze tena?

Kuna maswali mengi ya kujiuliza sasa.

Unapokua kipindi cha Ujana unaweza kufanya Mabadiliko Mengi sana ambayo yanaweza kuleta matoke chanya kwenye kipindi cha Ukomavu wa Jambo lolote.Hakikisha unafanya maamuzi yalio Sahihi kwenye Jambo lolote..hakuna Muujiza...hapa...Hata Uwapo unataka kukuza kiwango chako cha Kufikiria vitu anza mwanzo na utsonga mbele taratibu hakuna Muujiza hapa...
Jambo Lolote linapofikia mwisho ndipo tunaona Matokea kutokana na hatu mbili zilizopita na Hapa ndio watu wengi tunatoaga hukumu ya Maswali Mengi sana na vitu vingi sana maishani mwetu....Katika yote ukumbuke hili...

Growing is a Process Not An Event

God Bless Y’All
+255719742559
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.