KWA TAARIFA YAKO HII NDIO TAKWIMU YA WANAUME WAKIKRISTO NA PICHA ZA NGONO

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka maoni yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.

                                                                                                                                                                              ©switched.com


KWA TAARIFA YAKO hii leo ni kuhusiana na tafiti iliyofanywa na kundi la Barna Group la nchini Marekani ambalo katika utafiti wake kupitia watu mbalimbali limegundua kwamba asilimia 77 ya wanaume wa Kikristo wenye miaka kati ya 18 hadi 30 huangalia picha za ngono angalau kila mwezi.

KWA TAARIFA YAKO katika utafiti huo uliofanywa katika jumla ya wanaume wa kikristo wapatao 388, utafiti huo umebainisha kwamba asilimia 36 ya wanaume huangalia picha za ngono kila siku huku asilimia 32 wakikiri kuzidiwa na uangaliaji wa picha hizo. Aidha kwa wanaume wenye umri wa kati , utafiti unaonyesha asilimia 77 huangalia picha za ngono wakiwa kazini na asilimia 64 uangalia picha hizo angalau kila mwezi, huku pia asilimia 35 wenye ndoa wamekuwa na mahusiano nje ya ndoa zao.

KWA TAARIFA YAKO kundi hilo limesema limetoa taarifa hiyo si kwa kuhukumu bali kulijulisha kanisa ni wapi pa kusimama na kutafuta njia ya kuondoa tatizo hilo ambalo limeonekana kukua kwa kasi miongoni mwa watu wanaomwamini Mungu. Kwa mujibu wa bwana Joel Hesch ambaye alifadhili utafiti huo yeye ni mwanzilishi wa huduma ya wanaume wanaotambuliwa Kibiblia. Amesema utafiti huo ni kujulisha tatizo lililopo kutokana na tatizo la mtandao (internet).

KWA TAARIFA YAKO utafiti huu ulikuwa huko nchini Marekani, je unadhani Afrika na mabara mengine duniani kuna shida kama hiyo? kikubwa wenzangu wanaume ni kumuomba Mungu na kuepukana na maswala ya kuwa kwenye mtandao kwa muda mrefu bila kuwa na sababu ya msingi maana hupelekea kujitambukiza kutumia mda huo kuangalia picha za ngono au mambo mengine yasiyojenga.

                                                                                                                                   ©Patheos.com
                                                                                                                                                                        ©dailymail

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo vinginevyo tukutane wiki ijayo.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.