KWA TAARIFA YAKO: SIRI YAFICHUKA WAPIGANAJI WA ISIS IRAQ NA SYRIA WANAOGOPA KUULIWA NA WANAWAKE

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka maoni yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.
Moshi ukiwa umetanda angani mapigano yanayofanywa na kundi la ISIS katika mji wa Kobane©Reuters/Umit Bekas
KWA TAARIFA YAKO taarifa iliyotolewa hivi karibuni na chombo cha kimataifa cha habari 'AFP' kuhusiana na mapigano yanayoendelea huko Syria na Iraq yakihusisha kundi linalojiita Islamic state of Syria and Iraq (ISIS) likivumisha taarifa zake kwamba linapigana ili kulinda dini ya kiislamu (ingawa mataifa mengi ya kiislamu yanalipinga kundi hilo), ni kwamba wapiganaji wa kundi hilo wanaogopa kuuliwa na wapiganaji wanawake.

KWA TAARIFA YAKO taarifa iliyotolewa na AFP iliyohojiana na wapiganaji wanawake wa kabila la kikurdi nchini Iraq, inadaiwa kundi hilo linaogopa kupigana na wanawake kuliko wanaume kwakuwa endapo watauliwa na wanawake basi ni tiketi ya moja kwa moja motoni na kwamba ikitokea hali hiyo inamaana wasahau kuhusu mbingu pamoja na ahadi waliyopewa na Allah ya kukabidhiwa wanawake bikra 72 kila mmoja.

KWA TAARIFA YAKO katika mahojiano hayo na na mtu anayeshughulika na haki za binadamu huko Syria amesema ingawa kuna imani kwamba kundi hilo limeweza kutawala nusu ya eneo la mji wa Kobane huku watu laki 160,000 wakiwa wamekimbia makazi, inadaiwa wanawake wengi wa Kikurdi wameitikia wito wa kwenda kupigana na kundi hilo wakiwa na nia ya kuwalinda wanawake wenzao ambao wamezungukwa na wapiganaji hao hatari.

KWA TAARIFA YAKO mmoja wa wafanyakazi wa kimarekani Ed Royce ndiye aliyeweka hadharani kuhusiana na woga wa wapiganaji hao wakati alipohojiwa na The New York Post mwezi september mwaka huu. Royce alisema ISIS wanaogopa kufia mikononi kwa wanawake kwakuwa sheria ya watu wanaojihusisha na mambo ya jihadi ni kwamba watakataliwa mbinguni na hata zawadi yao ya bikra 72 hawataipata, ila itawezekana kupata ahadi hizo watakapoingia mbinguni endapo watafia vitani ila wakipigana na wanaume wenzao tu.

KWA TAARIFA YAKO mwanzoni maw mwezi hue octoba mpiganaji mmoja msichana kutoka kikosi cha peshmerga alikwenda nje kidogo ya mji wa Kobane walikokuwa wapiganaji wa ISIS kisha kuwarushia mabomu ya kurusha kea mono yaliyowaua wapiganaji wengi kisha msichana huyo alijimaliza mwenyewe kea kujilipua kea bomu. Kwa mujibu wa kamanda anayesimamia mapigano aitwaye Ahmed Rashid amesema kumekuwa na kundi kubwa la wanawake wanaojitokeza kupambana na ISIS wakiwa na lengo la kuwalinda wanawake wenzao waliopo maeneo yenye vita.

KWA TAARIFA YAKO kamanda huyo amesema kundi hilo la wanawake si jipya limekuwepo toka mwaka 1996 enzi za rais wa Iraq marehemu Saddam Hussein. Amesema wanawake hao wamekuwa wakipewa mafunzo na SWAT pamoja na vikosi maalumu kwenye masuala ya mapigano na kwamba tayari baadhi ya wanawake wameshiriki mstari wa mbele na wanaume katika vita na maadui zao, kwasasa anapanga kulituma kundi hilo mji wa Kirkuk hivi karibuni.

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo...

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.