TUMAINI [SHANGILIENI] WAVAMIA UMASAINI JIMBONI KWA LOWASSA KIINJILI

Mchungaji Andrew Kajembe wa St James pamoja na Askofu Stanley Hotay wakiwa ibadani.

Kwaya kongwe nchini ya Tumaini (Shangilieni) kutoka kanisa la Kianglikana la Mtakatifu James Kaloleni Arusha, siku ya jumapili wakiongozana na askofu wao mkuu wa dayosisi ya Mount Kilimanjaro walivamia jimboni kwa mheshimiwa Edward Lowasa kwa huduma ya ibada ya kipaimara pamoja na harambee ya kuchangia ununuzi wa kiwanja cha kanisa Anglikana Monduli chini.

Ibada hiyo iliyofana, jumla ya takribani milioni 6 zilipatikana kwakuanzia huku pia kwaya hiyo nayo haikuwa nyuma katika kuwezesha huduma ya Mungu kwa watu wa Monduli kusonga mbele.
 Kwaya zilizoshiriki katika tukio hilo ni pamoja na kwaya ya Umaki kutoka St.James ikiwa na Solo mkongwe wa Tumaini enzi hizo Mama Mhina, Kwaya ya Vijana wa Kimasai kutoka Monduli chini,pia kwaya ya Kanisa la Anglikani kutoka Monduli juu chini Msereji iliyokonga nyoyo za waumini na kuwabariki kwa uimbaji wao uliochangamka sana.

Kanisa la Mtakatifu James na Kanisa kuu [Christ Church] lilipo Arusha mjini ndio walezi wa makanisa takribani manne yalioyoko umasaini, likiwemo, Meserani A, Meserani B, Monduli Chini na Monduli Juu, chini Msereji, yote yakiwa ni uzao wa Mtakatifu James Anglikana na kanisa kuu Christ Church,na Clement Njamasi akiwa muinjilisti mzawa aliyetoa maisha yake kutumika Umasaini akisaidiwa na Musa Tobiko ambaye ni Mmasai,na sasa hivi yuko chuoni akisomea uinjilisti kwa ngazi ya cheti.

Pamoja na hayo ibada iliongozwa na Mchungaji Canon Kajembe na wachungaji wengine waliokuwepo katika ibada hiyo.Lakini pia kanisa linahitajika kumuombea injinia Sebiga ambaye ni injinia wa wilaya ya Monduli kwa jinsi alivyojitoa kutumika katika kanisa bila kujali cheo chake.

Askofu Stanley Hotay akihubiri.
Askofu Stanley Hotay wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro akisisitiza Jambo katika Mahubiri yake yaliyojaa mifano yenye mafundisho kwa kizazi cha Leo.
Wahitimu wa darasa la kipaimara wakiwa wamejipanga tayari kubarikiwa.
Taratibu za ubarikio zikiwekwa sawa huku wahitimu wakiwa wamepanga mstari.
Hii ni sehemu ya Ibada ya Kipaimara iliyofanyika Umasaini,Askofu Stanley Hotay akiwawekea mikono wahitimu wakimasai.

Wahitimu wa Kipaimara wa Jamii ya Kimasai wakiwa wamesimama kikakamavu ndani ya Yesu baada ya kuwekewa Mikono na Askofu Stanley Hotay.
Kwaya ya Monduli chini juu Msereji.
Hii ni Kwaya ya Monduli chini juu Msereji wakiongozwa na Soloist wao matata sana ( mfupi mwenye Masai shuka nyekundu)Wakimtukuza Mungu.
Sehemu ya waimbaji wa Kwaya ya Vijana wa kimasai wakifuatilia Ibada.

Baadhi ya waimbaji wa Kwaya ya TUMAINI wanashangilieni wakiwa ibadani Umasaini.
Waimbaji wa TUMAINI wakiwa wamezama Kwenye Maombi,katika Ibada huko Umasaini Monduli chini.
Maombi yakiendelea. 
Kwaya ya Vijana wa Kimasai.
Hii ni sehemu ya Kiwanja cha Kanisa ambacho Ibada ilifanyika ,kwa kufunga mahema ili Mungu atukuzwe,wanaooneka mbele na Masaani Shula nyekundu ni baadhi ya Watoto wa Kipaimara.
Sehemu ya Umati wa Waumini wakiwa ibadani huko Umasaini. habari pamoja na picha kwa msaada wa mdau wetu na ripota wa GK mkoani Arusha Bro Samuel Kusamba.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.