LICHA YA TISHIO LA KUUWAWA, WAKRISTO WAENDELEA KUJITOKEZA HADHARANI IRAQ

Baadhi ya waumini nchini Iraki wakiwa ibadani 
Licha ya tishio la kuuwawa kwa wakristo huku ikielezwa wapiganaji wa kundi la ISIS - Islamic State of Iraq and Syria, nchini Iraki wanakaribia kuingia mji wa Baghdad, wakristo waliopo jijini humo wameendelea kuonyesha imani thabiti baada ya familia moja kuamua kubatizwa ili kutimiza kusudi la imani yao kwa Muumba.

Kwa mujibu wa Kanon Andrew White wa kanisa Anglikana aliyepo nchini Iraki amesema wakristo waliopo Baghdad bado wameendelea kujitokeza kubatizwa licha ya hali ya hatari kutoka kundi la ISIS. Kupitia ukurasa wake wa Facebook Kanon Andrew ameandika licha ya tishio kubwa linalowazunguka bado wanaona uwepo wa utukufu wa Mungu, amesema walikuwa na furaha sana siku ya jumapili iliyopita baada ya kumbatiza mama mmoja pamoja na watoto wake wanne lakini kama haitoshi amesema furaha yake iliongezeka baada ya kufuatwa na mtoto wa miaka 10 baada ya ibada na kumweleza kwamba baada ya kubatizwa anajisikia kiumbe kipya kwasasa tofauti na alivyokuwa awali.


Kanon Andrew amesema familia hiyo ilikuwa inahitaji sana kuonyesha imani waliyonayo licha ya machafuko yanayoendelea nchini humo. Unaweza kusoma walichotenda wapigaji wa ISIS kwa kubonyeza HAPA

Mchungaji Kanon Andrew White.
Kanon Andrew White akiwa na wafanyakazi wa Foundation for Relief and Reconciliation mashariki ya kati yeye akiwa rais wa mfuko huo. Picha zote kwahisani ya ©frrme.org
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.