MAANDALIZI TAMASHA MWANZA SAFI, MAMBO YOTE SAA NANE MCHANA GOLDEN CREST

Ni usiku mkali, lakini ndio wakati muafaka wa kufunga vyombo kwa ajili ya asubuhi kila kitu kuwa sawa, na hapa tesing mbili tatu zinafanyika. Kisha asubuhi kuwe na testing nyingine ya mwisho. Lakini pamoja na hayo ushirika na waumini wa Mwanza ni muhimu, hivyo timu kutoka Arusha itakuwa na ibada kwenye makanisa mbalimbali, huenda wakatua kanisani kwako.

Takribani watu zaidi 1000 ndani ya Golden Crest jijini Mwanza watapata fursa ya kumsifu na kumuabudu Mungu kuanzua saa nane mchana. Na kama kuna sehemu ambapo binafsi (Elie) nilitamani kuwepo, basi ni Mwanza kwa wakati huu,

Interviews na vya habari mbalimbali zimefanyika,, na siku ya Ijumaa kulikuwa na mkesha ambao watu zaidi ya 150 walikuwepo kwenye mkesha huo, ambao hapo awali ilidhaniwa kwamba itakuwa ni kama sehemu ya kufanya mazoezi, lakini hali ikawa tofauti kwa idadi ya watu waliojitokeza, na hivyo kuwa ibada kamili ambapo Mungu alifanya kazi yake akiponya kila aliyekuja tofauti.

Kilichobakia muda huu ni kuandaa moyo wako tu, mara baada ya ibada kanisani kwako, kifuatacho ni sifa na kuabudu pale Golden Crest kuanzia saa nane mchana. Uina sababu ya kukosa? Basi zifuatazo ni picha za mazoezi ya Mise Anael na kundi lake, na tayari pamoja na Voice of Triumph, na wenyeji wengine wa Mwanza kuwepo, tayari Miriam Lukindo wa Mauki amefika kwa surprise, GK imefahamu. Mwingine nani ata-surprise? Fika ujionee mwenyewe.
Kifuatacho ni kipande cha video ujionee mfano wa mambo yatakavyokuwa, unapochanganya Saxophone na praise team.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.