MAKOSA YAKO YA JANA NDIO MAFANIKIO YAKO YA LEO

Hakuna mtu ambaye ameishi kwenye sayari hii katika siku zote za uhai wake bila kukosea kwenye jambo lolote. Mafanikio yote tunayoyaona leo yametokana na makosa mengi ambayo watu waliyafanya siku za nyuma. Yaani, kwa maana nyingine hatuwezi kujua tumepatia juu ya jambo fulani bila kujua kutokupatia kuna sura gani. Ili shilingi ijulikane ni shilingi lazima iwe na pande mbili. Hakuna shilingi ambayo siku zote ina upande mmoja tu, ndivyo pia maisha yalivyo.
Faraja Naftal Mndeme

Ukisoma Historia za watu mbalimbali maarufu na mashuhuri utakuja kukuta hapo mwanzo walikosea sana juu ya kile walichokuwa wanakifanya, na baada ya kugundua kwamba wamekosea ndipo hujaribu kufanya marekebisho kwanza kuleta muonekano bora juu ya jambo waliloliamini kuwa ni sahihi.

1. Makosa Uliyoyafanya Wewe Binafsi.
Kukosea ni sehemu ya maisha lakini sio maisha yote, Unapogundua umekosea unanyanyuka na kuendelea mbele. Makosa yako binafsi ni moja ya walimu wazuri waliokufundisha, ndio maana leo upo hivyo ulivyo. Hauwezi kuishi zaidi ya makosa ambayo uliyoyaona kwako binafsi.

Kama uliwahi kufukuzwa kazi kwa sababu umekosea kufanya jambo fulani kwa uangalifu, siku unapopata kazi mpya unajitahidi sana kile kilichokufukuzisha kazi usikirudie tena. Iwapo Kuna wakati huwa tunatumia hela zote bila kujali siku unapopatwa na dharura inayohitaji fedha ya muhimu sana, na wewe fedha zote ulitumia vibaya inakufundisha kwamba siku ukipata fedha nyingi lazima kuna kutunza kiasi fulani cha fedha - ili hata iwapo dharura itatokea tena usiaibike. 

Usiogope kukosea maana makosa yako ya leo ndio yanakusaidia kutengeneza maisha yako ya kesho. Iwapo tusingejua maisha ya dhambi yakoje  na matokeo yake hapa ulimwenguni tusingejua hata Mungu anafananaje kwenye maisha yetu ya kila siku.

Mwanzuoni mmoja aliibuka na kusema kwamba kama haukuwahi kukosea juu jambo lolote basi tambua kwmba haukuwahi kujaribu kitu kipya kwenye maisha yako.


2. Makosa ya Watu Wengine.
Wahenga walisema ukiona mwenzio ananyolewa nywele basi wewe weka maji Kichwa. Unapofanikiwa kumuona Mtu anakata mti na panga butu halafu akashindwa kumaliza kazi kwa wakati, basi wewe kesho ukitaka kukata mti utajifunza kulinoa panga hilo. Hakuna mtu ambaye ana uwezo wa kuishi na kufanya kila kitu na kujifunza kwa makosa ya kwake binafsi. Tunawahitaji wengine ili kuweza kujifunza. Makosa ya mtu mwingine leo ndio Mafanikio yako ya kesho.

Ukiona mtu amefilisika na matumizi mabaya yake ya fedha na kushindwa kuendesha miradi aliyoianzisha - siku zote utatumia makosa ya mtu yule kama sehemu ya rejeo ili kutoweza kufanya makosa aliyoyafanya hadi kupelekea matokeo mabaya. Mara nyingi watu waliojifunza kusikiliza na kuangalia makosa ya wengine juu ya jambo fulani kwa umakini, wamekuwa na mafanikio zaidi kwenye jambo husika kuliko hata yule ambaye amewahi kukosea. Tunawahitaji wengine ili kuweza kuendelea mbele.

Mwisho wa siku tunaendelea kusema, epuka kuishi kwenye makosa yaliyopita lakini yatumie makosa kama mwalimu wako. Yaliopita si ndwele lakini tugange yajayo. Usiogope kukosea, jaribu kufanya vitu vipya, kukosea ni sehemu ya maisha. Maisha ni safari ambayo haina mjuzi bali wote tu wanafunzi kwenye kila jambo. Ishi ndoto zako, jaribu kutafuta fursa mpya za maisha na jaribu kuzitumia bila woga kwa sababu Makosa yako ya Jana ndio Mafanikio yako ya Leo.

God Bless Y'All
+255719742779
 +255719742779

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.