MWANAMKE MPIGANAJI SYRIA ATOROKA BAADA YA KUSHUHUDIA MWANAUME AKICHINJWA

Wanajeshi wa kundi la ISIS wakiingia kwa maandamano ya magari mitaa ya mji wa Raqqa June 30 mwaka huu kusherehekea kutawala mji jirani nchini Iraq©Reuters

Mwanamke mmoja ambaye alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi nchini Syria na mpiganaji mstaafu wa kundi hatari la wanamgambo wanaojiita Islam state (ISIS) linalopigana nchini Iraq na Syria, amelikimbia kundi hilo baada ya kushuhudia mtoto akisulubiwa vikali ikiwa pamoja na mwanaume kukatwa kichwa mbele yake.

Mwanamke huyo anayetumia jina la Khadija (25) , amesema anataka kuweka wazi unyama unaofanywa na kundi hilo ili wanawake wote wanaojiunga na kundi hilo kwakudanganywa kwamba wanatetea dini waache kufanya hivyo kwakuwa kundi hilo halijasimama kwa mlengo wa kutetea dini bali unyama na ukatili dhidi ya binadamu wenzao. Akihojiwa na kituo maarufu cha runinga duniani CNN ameeleza namna alivyodanganywa mpaka kujiunga na kundi hilo na namna alivyoweza kutoroka akipitia Uturuki kabla ndege za kivita za Marekani hazijaanza kushambulia mwezi Septemba.

"Sitaki mwanamke yoyote adanganyike na kundi la ISIS, kwakuwa wasichana wengi wanajiunga wakidhani ni waislamu safi, alisema mwanamke huyo akitumia jina la Khadija. Amesema alijikuta akivutiwa kujiunga na kundi hilo kupitia mwanaume Mtunisia aliyekutana naye kwa njia ya mtandao wa mapenzi (online dating), amesema mwanaume huyo alikuwa akimshawishi sana kujiunga na kundi hilo kwakuwa ni jambo sahihi na kwamba alimtaka wakutane huko Raqqa (mji mmoja wapo huko Syria).

Khadija amesema mwanaume huyo alimwambia kundi hilo sio la kigaidi na kwamba sio baya kama inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari, akasema akatiwa moyo na mwanaume huyo kwakuambiwa kwamba lengo kubwa la kundi hilo ni kueneza uislamu wa kweli na kwamba kundi hilo litapunguza vitendo vya mapigano mara tu vita itakapoisha. Khadija amesema kitendo cha kumuamini moja kwa moja mwanaume huyo kwa njia ya mtandao, Khadija aliilazimisha familia yake kwamba wanahamie Raqqa kwakuwa ni uamuzi mzuri kwa faida ya wadogo zake ambaoalikuwa akihitaji kuwaandikisha shule.

Mmoja wa ndugu wa Khadija alikuwa akiishi Raqqa na bila kutegemea naye alikuwa mmoja wa wapiganaji wa ISIS kitengo cha Khansa'a ambacho kimeundwa na wanawake 30 ambao kazi yao ni kufanya doria mitaa ya Raqqa na kumwadhibisha mwanamke yeyote ambaye hajavaa vizuri mavazi yake kwa mujibu wa sheria ya kiislamu, na kwamba adhabu kubwa kwa kitendo hicho ni bakora.

Amesema mara baada ya kuhamia Raqqa na kukutana na ndugu yake alimchukua hadi makao makuu ya wapiganaji hao na kumtambulisha kwa kiongozi wao aitwaye Umm Rayan. Khadija alitakiwa baada ya kujiunga afundishwe namna ya kutumia bastola. Ingawa Khadija alikuwa na hali ya furaha kwa kujiunga na kundi hilo lakini furaha yake ilibadilika na kuwa mtu wa kuogopa. "Tulikwenda mtaani kwa doria na tulipomuona mwanamke hajavaa inavyotakiwa tulimkamata na kumchapa fimbo, mwanzoni nilikuwa na furaha, nilikuwa nabeba bunduki, kilikuwa kitu kipya kwangu, nilikuwa na mamlaka bila kudhani nilikuwa nawaogopesha watu. Lakini nikaanza kujiuliza maswali, nipo wapi? naenda wapi? nilikuwa najisikia mawimbi yakinivuta sehemu mbaya" amesema Khadija.

Akaanza kawa na mashaka baada ya kuona baadhi ya wapiganaji wa kigeni walivyokuwa wanawatendea wake zao, akakumbuka namna mwanamke mmoja alivyopigwa vibaya na kuchukuliwa chumba cha dharura. Amesema makao makuu pia kulikuwa na chumba kilichokuwa kikitumika kusikiliza mashtaka ya ndoa na mda mwingine kulazimisha ndoa. Khadija amesema alianza kufikiria upya kwanini alifikia uamuzi wa kujiunga na kundi hilo baada ya kugundua mauaji yao ya kinyama.

Anasema tukio la kwanza kushuhudia kwa macho yake ni kusulubiwa kwa kijana mmoja na wapiganaji wa ISIS akituhumiwa kubaka, lakini tukio la mwisho ni pale aliposhuhudia mwanaume akichinjwa mbele yake. Muda mfupi baada ya kushuhudia tukio hilo, kiongozi wake aitwaye Rayan alianza kumlazimisha waanze mipango ya yeye kuolewa na ndipo alipojigundua kwamba anahitaji kutoroka. "Hapo ndipo niliposema sasa basi, kwayote niliyoshuhudia na mda niliokaa kimya, nikajiambia tupo vitani. baada ya haya nikaamua hapana sasa nahitaji kuondoka.

Kwasasa Khadija yupo Uturuki akijaribu kurudisha maisha yake kama ilivyokuwa zamani ingawa anaogopa ISIS labda wamemweka katika alama ya watu wanaotakiwa kuuwawa kwa uamuzi wake wa kutoroka. Pia familia yake imehama mji wa Raqqa ingawa bado wapo nchini Syria, Khadija anataka maisha yake yarudi kama yalivyokuwa mwanzo. "Msichana aliyeolewa, anayependa maisha yake na kufurahi…anayependa kusafiri, kuchora, kutembea mtaani akiwa na spika zake masikioni akisikiliza muziki bila kujali watu wengine wanamfikiriaje, ndivyo ninataka niwe kwa mara nyingine." amesema Khadija.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.